loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mafanikio 14 ya Mapinduzi Zanzibar

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, ameelezea mafanikio yaliyofi kiwa visiwani humo, tangu kufanyika kwa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 pamoja na mafanikio yaliyofi kiwa katika kipindi cha miaka tisa ya utawala wake tangu mwaka 2010.

Alisema hayo jana Visiwani Zanzibar wakati wa Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani. Maadhimisho hayo, yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, akiwemo Rais Dk John Magufuli na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Bashiru Ally, Mama Fatma Karume, mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye na viongozi wengine mbalimbali wa chama na serikali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali.

Akiwahutubia wananchi uwanjani hapo, Dk Shein alianisha mambo 14 kama sehemu ya mafanikio yaliyofikiwa katika Awamu zote Saba za Serikali za Mapinduzi Zanzibar tangu mwaka 1964. Alisema wananchi wanapaswa kutambua kwamba Mapinduzi yaliyofanyika Januari 12, 1964 visiwani humo, yalilenga kuondoa dhuluma na kuleta uhuru wa kweli wa Zanzibar na watu wake, kupinga ubaguzi na kuleta umoja, mshikamano na usalama.

Dk Shein aliwataka wananchi kuendelea kuwaenzi waasisi wa Mapinduzi hayo, wakiongozwa na Hayati Abeid Amani Karume, pia wathamini amani na utulivu na kufuata sheria za nchi, kwa kuwa uvunjifu wa amani, unatokana na watu kutotii misingi ya sheria.

“Tuna wajibu wa kuyatambua na kuyathamini Mapinduzi yetu ambayo yalikata minyororo ya ubaguzi na aina zote za dhuluma dhidi ya wafanyakazi na wakulima wa Zanzibar, yalifungua ukurasa mpya wa maendeleo ya Zanzibar na watu wake, hivyo hatuna budi kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi akiwemo Mzee Abeid Amani Karume na viongozi wengine,”alisema.

Kutokana na hilo, alisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zitaendelea kuudumisha Muungano kwa dhamira ileile iliyokuwemo kwa Waasisi wa Muungano huo, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Dk Shein pia aliwakumbusha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia, kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, pale muda utakapofika ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka kwa maendeleo yao na taifa.

Mafanikio yaliyofikiwa

Katika kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Shein alisema Zanzibar imepata mafanikio mbalimbali katika sekta zote.

Kwamba mafanikio hayo yanatokana na sababu za msingi za Mapinduzi hayo, ikiwemo umoja, mshikamano na usalama kwa wananchi wote. Alisema tangu mwaka 2010, Serikali yake ya Awamu ya Saba iliendelea kutekeleza mipango mikuu ya kiuchumi, ikiwemo Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUZA) katika awamu zote tatu za mpango huo, utekelezaji wa Ilani ya CCM, Dira ya Maendeleo ya 2020 na utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa ushirikiano na taasisi za kimataifa.

Kwa mujibu wa Dk Shein, katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, uchumi wa Zanzibar umeendelea kustawi na kuimarika. Alisema kustawi na kuimarika kwa uchumi huo, kumechangiwa na uwepo wa amani na utulivu. Kwamba Pato la Taifa limeongezeka kutoka Sh milioni 1,768 mwaka 2010 hadi kufikia Sh milioni 2,874 mwaka 2018.

Mafanikio mengine ni ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 4.3 mwaka 2010 hadi asilimia 7.1 mwaka 2018, kuongezeka kwa pato la mwananchi kutoka Sh 942,000 mwaka 2010 hadi kufikia Sh milioni 2.4 mwaka 2018. Mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 14.7 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 3.9 mwaka 2018, hali inayowafanya wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu.

“Uchumi wetu umeimarika na kusababisha kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani. Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, mapato ya ndani yalikuwa shilingi milioni 748.9 ikilinganishwa na shilingi milioni 181.1 mwaka 2010/2011, utegemezi wa bajeti nao umepungua kutoka asilimia 30.2 mwaka 2010/2011 hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka 2018/2019,”alieleza Dk Shein.

Kuhusu uwekezaji, alisema umezidi kuimarika kwa kuwa hadi mwaka 2018 miradi ya maendeleo 304 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3.74 ilitekelezwa na kutoa ajira 16,866 kwa wananchi Mpango wa elimu bure ulioasisiwa tangu Septemba 23, 1964, umeendelezwa kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Sh bilioni 47.93 mwaka 2010/2011 hadi kufikia Sh bilioni 178.917 mwaka 2019/2020.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa shule na taasisi za elimu na wanafunzi katika ngazi mbalimbali, matibabu bure na kuboreshwa kwa maslahi ya wafanyakazi na utumishi wa umma.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 16 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...