loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtibwa, Simba ni fainali ya kisasi Mapinduzi leo

FAINALI ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuchezwa leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kwa kuzikutanisha Simba na Mtibwa Sugar kuanzia saa 2:15 usiku.

Simba ilifuzu fainali baada ya kuifunga Azam FC ambayo ilikuwa bingwa mtetezi kwa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu na Mtibwa Sugar ikaotoa Yanga kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1.

Katika historia ya michuano hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2007, Simba imetwaa ubingwa mara tatu ambapo mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ni mwaka 2015 kwa kuifunga Mtibwa Sugar Simba na Mtibwa Sugar zimewahi kukutana fainali mwaka, 2008 na 2015 na mara zote Simba ilishinda hivyo mchezo wa leo kila timu itakuwa inahitaji kuandika historia yake.

Mtibwa Sugar imewahi kutwaa ubingwa wa Mapinduzi mara moja mwaka 2010 baada ya kuifunga Ocean View ya Zanzibar lakini imefika fainali mara sita huku Simba ikicheza fainali mara saba na kutwaa ubingwa mara tatu.

Akizungumza kocha msaidizi wa Simba, Suleman Matola alisema anaamini mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu kila timu ina wachezaji wazuri na kila timu inahitaji kutwaa ubingwa ili andike historia ya mapema mwaka 2020.

“Tunajua mchezo utakuwa na ushindani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili tuwe bingwa kwani kuna raha ya kuanza kuandika historia ya kombe la kwanza mwaka 2020 mapema,”alisema Matola Naye kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alisema malengo yao ni kutwaa ubingwa hivyo wamejipanga kuhakikisha malengo yao yanatimia “Tumejiandaa vema na malengo yetu ni kutwaa ubingwa hivyo tunaomba Mungu atuamshe salama ili tukafanikishe lengo letu,” alisema Katwila Mashindano haya ya 13 yalishirikisha timu nne za Zanzibar ambapo zote zimeaga mashindano na timu nne za Tanzania Bara na yanachezwa kwa mtindo wa mtoano ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka Sh Milioni 15 pamoja na Kombe.

Timu ambazo zilishiriki mashindano kutoka Kundi A ni na tayari zimeaga mashindano ni Yanga, Mlandege na Jamhuri na Kundi B ni timu za Azam FC, Zimamoto na Chipukizi.

Mashindano hayo maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi yalianza mwaka 2007 na hufanyika kila mwaka na mwaka huu yalichezwa kwa mtindo wa mtoano.

Orodha ya Mabingwa Kombe la Mapinduzi.

2007.Yanga

2008. Simba

2009. Miembeni

2010. Mtibwa Sugar

2011.Simba

2012.Azam FC

2013. Azam FC

2014.KCCA

2015. Simba

2016. URA

2017. Azam FC

2018. Azam FC

2019. Azam FC

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi