loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shime aipania Burundi

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, Bakari Shime amesema atacheza mchezo wa kushambulia muda wote wakati watakaporudiana na Burundi mwishoni mwa mwezi huu Bujumbura, Burundi.

Timu hiyo ya Tanzania juzi iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Shime ‘Mchawi Mweusi’ametoa kauli hiyo juzi mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, ambao matokeo yake yameiweka pazuri Tanzania kusonga hatua inayofuata.

Shime kikosi chake kinalazimika kulinda ushindi huo dhidi ya Burundi, huku akibainisha kuwa timu yake itacheza soka la kushambulia na sio kujilinda ili wapate mabao zaidi na kuwafanya Burundi kutoliandama lango la Tanzania na baki kujilinda.

“Tunajua mchezo wa marudiano utakuwa mgumu kwakuwa tutakuwa ugenini, lakini naamini nitatumia mbinu ya kushambuliana muda wote ili kuendelea kuongeza idadi ya mabao kuwachangaya wapinzani wetu na wasahau kutushambulia,“ Shime Kwa upande wake kocha wa Burundi Niyibimenya Daniella alisema kwenye mchezo huo kikosi chake kilizidiwa ndiyo sababu iliyochangia kupoteza mchezo huo kwa mabao mengi.

Alisema anaamini bado wana nafasi ya kujirekebisha kwenye kipindi kilichobakia na kupindua matokeo wakiwa kwao ili kutinga hatua inayofuata.

“Wachezaji wangu walizidiwa muda wote hasa kipindi cha kwanza na hiyo ilitokana na wachezaji wengi kushindwa kujiamini na walipoenda kwenye mapumziko niliwarekebisha na walirejea uwanjani wakiwa tofauti na kufanikiwa kuzuia kasi ya wenyeji wetu kufunga, “ alisema Daniella.

Mshindi wa jumla kwa michezo yote nyumbani na ugenini atafanikiwa kusonga mbele na kumsubiri mshindi kwenye mchezo kati ya Uganda dhidi ya Ethiopia na mshindi wa hapo atajihakikishia kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia inazotarajiwa kufanyika nchini India mwaka huu.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi