loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mamba aua mwanafunzi, ng’ombe 20 wapigwa radi

WATU wawili wamefariki dunia, akiwemo mwanafunzi wa Kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari Kabwe mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa, Michael Kanyeta (18) aliyeuawa na mamba, huku zaidi ya ngo'mbe 20 wamekufa baada ya kupigwa na radi.

Mizoga 20 ya ng'ombe ilishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi - Afya), Dk Dorothy Gwajima ikiwa imetapakaa katika bararaba kuu inayounganisha miji ya Sumbawanga (Rukwa) na Mpanda (Katavi ) katika kijiji cha Kantawa wilayani Nkasi, umbali wa kilomita 25 kutoka mji wa Namanyere.

Tukio hilo lilitokea wakati Dk Gwajima aliyekuwa mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, akisafiri kutoka Namanyere akielekea mjini Sumbawanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Justine Masajo akizungumza na gazeti hili alithibitisha vifo vya watu hao wawili vilivyotokea wilayani Nkasi. Alisema hakuna kifo chochote cha binadamu, kilichotokea katika tukio hilo la kuuawa ngo'mbe 20 kwa kupigwa na radi.

Alisema mvuvi, Onso Kina (25) mkazi wa Kata ya Korongwe, alikufa wakati akivua samaki na wenzake katika Ziwa Tanganyika upande wa Kata ya Kabwe. Mwingine ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili, Michael Kanyeta (18) aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari Kabwe, ambaye aliuawa na mamba akiwa anafua sare zake za shule ziwani.

Akizungumza na gazeti hili Diwani wa Kata ya Kabwe mwambao mwa Ziwa Tanganyika, Asante Lubisha alisema mwanafunzi huyo, Kanyeta, Januari 10 mwaka huu mchana akiwa anafua sare zake za shule ziwani, ghafla alishambuliwa na kuuawa na mamba.

"Kwa msaada wa wanakijiji cha Kabwe mwili wake ulipatikana na kuopolewa ziwani, maziko yake yalifanyika juzi. Kwa takwimu tulizonazo watu waliouwawa na mamba katika Kata ya Kabwe wamefika 14 tangu 2010 hadi sasa, kati yao wanne waliuawa mwaka uliopita,"alieleza.

Akisimulia mkasa mwingine, alisema mvuvi akiwa anavua samaki katika Ziwa Tanganyika upande wa Kata ya Kabwe, ghafla hali ilibadilika na kusababisha mawimbi makubwa.

"Mtumbwi wao ulipinduka na kuwamwaga wavuvi hao ziwani, walikuwa watatu lakini waliweza kuubinua mtumbwi wao na kuingia ndani. Kina aliyekuwa amevaa kandambili, aliziona zikielewa ziwani akapiga mbizi kuzifuata. lakini aliishiwa pumzi akafa," alieleza Diwani Lugwisha.

Ofisa habari Atley Kinu aliyekuwa kwenye gari la Naibu Katibu Mkuu – Tamisemi (Afya), Dk Gwajima alilielleza gazeti hili kuwa tukio la kushuhudia mizoga ya ng'ombe ikiwa imezagaa barabarani, liliwashitua na kuwa na hofu kubwa. Akizungumza na gazeti hili, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Kasululu amewatahadharisha wananchi kujiepusha na kula mizoga ya wanyama, ambao wamekufa kwa kupigwa na radi, kwamba wanaweza kudhurika kiafya .

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Fredy Siyame, Sumbawanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 16 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...