loader
Picha

Maagizo manne ya Rais kwa mabalozi walioapishwa leo

Rais John Magufuli amewaapisha mabalozi wanne, leo, Jumanne, Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akiwaagiza kutengeneza fursa za ajira kwa vijana katika vituo vyao vya kazi.

Walioapishwa ni pamoja na Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania huko Afrika Kusini, Dk Modestus Kipilimba (Namibia), Profesa Emmanuel Mbennah (Zimbabwe) na Dk Benson Bana (Nigeria).

Katika tukio hilo, Rais Magufuli amewapongeza mabalozi hao na kuwaambia kuwa nchi wanazokwenda zina fursa nyingi katika kujenga taifa la Tanzania lenye muelekeo mpya wa maendeleo ya watu wake.

“Nendeni mkafanye kazi, simamieni uchumi, simamieni taifa, katengenezeni nafasi za ajira kwa Watanzania walioko huko,” ameongeza.

Aidha ameongeza kuwa anatamani ndani ya wiki mbili mabalozi hao wawewamekwisha ripoti kwenye vituo vyao vya kazi walivyopangiwa ili kuanza kazi.

SERIKALI itajenga hospitali ya kisasa mjini Chato itakayokuwa hospitali ya ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi