loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanasiasa walivyochambua uhuru bandia wa 1963 Z’bar

VIJANA wa Zanzibar wanatakiwa kutambua kwamba Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 ndiyo yaliyomkomboa mwananchi na sio uhuru wa Desemba 10 mwaka 1963 kama ambavyo wameanza kujitokeza baadhi ya watu wakidai.

Hayo yanasemwa na Waziri wa Vijana, Utamaduni na Sanaa, Ali Karume wakati akihutubia kongamano la Vijana katika kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdull Wakil mjini Unguja.

Jumapili iliyopita, Wazanzibari waliadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi, sherehe ambazo zilihudhuriwa pia na Rais John Magufuli. Waziri Karume anasema uhuru wa Desemba 10 mwaka 1963 haukuwa uhuru wa kweli kwa wananchi wazalendo wa Zanzibar kwa sababu ulikuwa bado unamtambua Sultani wa Oman kama mtawala.

Anafafanua kwamba uhuru huo haukutolewa kwa lengo la dhati la kuwafanya wazalendo kuwa huru katika nchi yao kwa kumiliki mambo muhimu ya msingi ikiwemo ardhi bali kuendelea kuwa watwana katika nchi yao.

Anakanusha kauli za baadhi ya watu ikiwemo wanasiasa wanaojaribu kuupa heshima uhuru wa Desemba 10 wa mwaka 1963 wakidai eti uliwalenga wananchi wa Zanzibar kuwa huru katika nchi yao.

‘’Mapinduzi ya 1964 ndiyo yaliyomkomboa mwananchi wa Zanzibar kuwa huru katika nchi yake... Uhuru wa Desemba ulikuwepo lakini uliwalenga watu wachache na makundi ya makabila fulani,” anasema. Anawataka Vijana kuyaunga mkono Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 kwa sababu miongoni mwa kundi ambalo limefaidika sanana na hatua hiyo ni vijana ambao wengi hawakuwpo wakati wa mainduzi hayo.

Anataoa mfano kwamba mara baada ya Mapinduzi, Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Karume alitangaza elimu kutolewa na serkikali bure kwa wananchi Septemba 23 mwaka 1964 na hivyo kutoa fursa kwa kundi kubwa la vijana kusoma katika shule mbali mbali zilizotaifishwa na serikali.

Aidha anasema wananchi walikuwa hawamiliki ardhi kwa ajili ya kujenga makazi wala kilimo, lakini mara baada ya mapinduzi ardhi ilitaifishwa na kuwa milki ya wananchi Baraka Shamte, kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye baba yake mzazi Mohamed Shamte ndiye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Desemba 10 anasema bila kumung’unya maneno kwamba serikali iliyoongozwa na baba yake ilikuwa kiini macho cha kutaka kuidanganya dunia kwamba Zanzibar ni huru.

Shamte anasema nchi haiwezi kuwa huru na wananchi wake kama utawala wa kigeni utaendelea kushika hatamu za uongozi na kuwakandamiza wazalendo.

Anasema hicho ndicho kilifanyika kwa uhuru wa Disembar 10 mwaka 1963 uliodaiwa kutolewa kwa wananchi huku ukweli ukiwa kwamba Sultani alikuwa anaendelea kushika hatamu za uongozi wa dola.

Anasema siasa za Zanzibar katika harakati za kisiasa zilikuwa zenye mwelekeo wa chuki na kuwagawa wananchi wake. ‘’Mimi baba yangu alikuwa Hizbu na kiongozi wa ngazi za juu akiwa Waziri Mkuu... Mimi nilitofautiana naye na nilikuwa (ASP) wa hali ya juu... Sikutaka kutawaliwa na kusikiliza kasumba za wapinzani.’’

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ussi Yahya ambaye alipata kufanya kazi katika Serikali ya Sultani kabla ya Mapinduzi anasema madhila na ukandamizaji wa wananchi kutoka kwa Sultani ndiyo yaliyowasukuma Wazanzibari kufanya Mapinduzi.

Anasema wapo watu wanajaribu kupotosha ukweli na kusema utawala wa Sultani haukuwa na madhara yoyote kwa wananchi wa Zanzibar jambo analosema ni mtazamo wa ajabu sana.

Anasema utawala huo unawezaje kuwa sahihi wakati umiliki wote wa ardhi kwa shughuli za kilimo na makazi ulikuwa ulikuwa chini ya Sultani pamoja na familia yake au ndugu wa karibu.

Kwa mfano, anasema Unguja na Pemba yalikuwepo jumla ya mashamba 745 ambayo yote yalimilikiwa na familiaa au ndugu wa Sultani. Anasema ilipofika tarehe Novemba 11, hayati Karume alianza kazi ya ugawaji wa ardhi katika mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na familia ya Kisultani kwenda kwa wananchi wazalendo.

‘’Karume aligawa eka tatu tatu kwa wananchi wazalendo ili kuzitumia kwa shughuli za Kilimo,’’ anasema. Ussi anasema kabla ya Mapinduzi alikuwa tarishi na alikuja kuajiriwa na kuanza masomo nje ya nchi mara baada ya Mapinduzi mwaka 1964.

Anasema kupitia serikali huru ya wazalendo, alikwenda China kusoma kuhusu namna ya kuendesha shughuli za kifedha na Benki.

‘’Nilipelekwa China kwa ajili ya masomo ya miaka miwili kuja kuanzisha Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ).’’

Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi, Khadija Jabir anasema wanawake kabla ya Mapinduzi walikuwa hawana sauti huku wakinyimwa haki ya kupiga kura katika chaguzi mbali mbali zilizopita.

Anasema Mapinduzi ndiyo yaliyofungua milango na kuwafanya wanawake kutambuliwa hadi kushika nafasi mbalimbali za uongozi. ‘’Mapinduzi ndiyo yaliyokuja kumpandisha hadhi mwanamke na kumtambua mwanamke na kumpa nafasi za uongozi,’’ anasema.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa anasema utawala wa Kisultani uliwanyima wananchi haki zote za msingi ikiwemo umiliki wa ardhi, elimu na masuala mengine ya kijamii.

Anasema kwa mfano katika kisiwa cha Pemba Ardhi yote yenye rutba ilikuwa ikimilikiwa na familia ya Sultani pamoja na mashamba ya mikarafuu.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Na Khatib Suleiman

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 17 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...