loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China yaadhimisha mwaka mpya wa panya Dar

KITUO cha Utamaduni wa China nchini kimeadhimisha mwaka mpya wa taifa hilo, jijini Dar es Salaam, ambao unafanana na sikukuu ya Krismasi katika nchi za Magharibi.

Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa China ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Wang Siping, kutokana na desturi ya Wachina sikukuu hiyo inaanzia Desemba 23 kwa kalenda ya Kichina hadi Januari 15.

“Katika siku hizo za mwaka mpya, siku ya mwisho yaani tarehe 30 ya mkesha wa sikukuu na siku ya kwanza ya Januari ni siku za sherehe, au kwa maneneo mengine siku hizi mbili ni kilele cha sikukuu ya Spring,” alisema.

Alisema kwa kalenda ya kilimo ya China, mwaka huu ni mwaka wa Panya, kutokana na utamaduni wa China, panya ni alama ya kiutamaduni wa kila kitu kizuri kwa sababu panya ni mwepesi, mtulivu, pia anajua kutunza nafaka kwa hiyo ni alama ya mali vile vile.

Naye Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini China, Abdulrahman Shimbo alisema sherehe hiyo inamaanisha ujio wa mwaka wa Kichina kwani takriban Wachina milioni 600 kutoka maeneo mbalimbali wanarudi nchini kwao kwenda kusheherekea.

Aliwataka Watanzania kudumisha utamaduni kwa kuwa ni muhimu katika taifa vile vile katika makabila barani Afrika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania walioishi na kusoma China, Dk. Liggy Vumilia alisema nchi hiyo ni rafiki mkubwa wa Tanzania kwani mahusiano yake yamekuwepo kwa miaka mingi ni fursa pekee ya kubadilishana utamaduni pamoja na kukuza mahusiano.

Alisema China inajifunza kutoka Tanzania kwani ina makabila zaidi ya 120 ilhali China makabila 56 hivyo inawezekana kukaa pamoja na kuzungumza lugha moja kwa amani na upendo.

MGOMBEA urais wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

Magufuli: Nataka kumalizia kazi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

MGOMBEA urais wa ...

Wanawake waihakikishia CCM ushindi

masaa 14 yaliyopita Magnus Mahenge, Dodoma

 

Waziri aagiza mifumo ya fedha ipunguze rushwa

masaa 16 yaliyopita Mwandishi Maalumu, Simiyu

WAZIRI ...