loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakenya wavunja rekodi za dunia

MSHINDI watatu wa dunia wa mbio za meta 10,000 Rhonex Kipruto na bingwa wa Afrika wa mwaka 2016 wa meta 5,000, Sheila Chepkirui wamevunja rekodi za wanaume na wanawake za barabarani za kilometa 10 katika mashindano yaliyofanyika hapa.

Kipruto mwenye umri wa miaka 20 alishinda mbio za Valencia Ibercaja za kilometa 10 za barabarani juzi Jumapili katika muda mpya wa dunia wa dakika 26 na sekunde 23.

Chepkirui, mshindi namba mbili wa mbio za nyika wa mwaka 2016, alimaliza kwa kutumia dakika 29:42 katika mbio za wanawake katika mbio hizo zilizofanyika katika jiji hilo la Hispania.

Kipruto, ambaye pia ni mshindi wa dunia wa meta 10,000 kwa wanariadha wenye umri chini ya miaka 20, aliweka muda mpya ikiwa ni wiki sita baada bingwa Mganda Joshua kushinda mbio za meta 10,000 wakati wa mashindano ya Nusu Marathoni ya Valencia Desemba mosi mwaka jana.

Kipruto alimaliza umbali wa kilometa tano kwa kutumia dakika 13:18 wakati akielekea kuvunja rekodi ya Cheptegei kwa sekunde 15. Cheptegei, bingwa wa mbio za nyika wa dunia, alivunja rekodi ya kilometa 10 za dunia huko Valencia, akiweka muda mpya wa dakika 26:38.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 Mganda alivunja rekodi ya awali kwa sekunde sita, ambayo iliwekwa na Mkenya Leonard Komon aliposhinda mbio za kilometa 10 za Utrecht Singelloop kwa muda wa 26:44 Septemba 26, 2010 huko Uholanzi.

Matokeo:

1. Rhonex Kipruto (Kenya) 26:24 (Rekodi ya Dunia)

2. Bernard Kimeli (Kenya) 27:12

3. Julián Wanders 27:13 (Ulaya)

Wanawake:

1. Sheila Chepkirui (Kenya) 29:42

2. Rosemary Wanjiru (Kenya) 29:46

3. Norah Jeruto (Kenya) 29:46

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: VALENCIA, Hispania

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi