loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga hesabu kali kwa Kagera

ULE uhondo wa kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea leo, kwa mabaingwa wa kihistoria, Yanga watakuwa na hesabu kali. Hesabu hizi ni za kuendeleza kampeni za kusaka nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa kutafuta ushindi dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Yanga wanaoshika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 12, hivyo wanaingia na hesabu kali za kutafuta pointi tatu muhimu ilikufikisha pointi 28 zitakazo wafanya kupanda hadi nafasi ya tatu , wanakutana na Kagera wanaoshika nafasi ya nane wakiwa nyuma kwa pointi 24 wakicheza michezo 16.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wa 13 wanaohitaji zaidi ushindi wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare kwenye mechi iliyopita dhidi ya mtani wao Simba kwa kufungana mabao 2-2.

Wanakutana na Kagera, ambao kwa siku za hivi karibuni wana mwenendo mbaya wa kusaka matokeo kwani michezo yao mitatu iliyopita ya ligi hiyo walipoteza ikiwemo ule wa Polisi Tanzania kwa mabao 2-1.

Yanga bado wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na kikosi chao kuwa na morali waliyonayo kufuatia kupata sare dhidi ya watani zao Simba, ambao wanaonekana kuwa na kikosi bora ikilinganisha na wao licha ya kwamba mchezo wa mpira unamatokeo ya ajabu.

Pamoja na hivyo, Yanga bado wanabebwa na rekodi ya kushinda michezo ya miwili ya msimu uliopita, ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga wakiwa ugenini walishinda mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati mechi ya mzunguko wa pili, Yanga walishinda mabao 3-2 mchezo ulifanika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Aidha, mchezo huo ni mtihani wa kwanza kwa kocha mpya wa Yanga Mbeligiji, Luc Eymael kukiongoza kikosi hicho toka amejiunga na miamba hiyo.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi