loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simbachawene awataka wawekezaji kufuata sheria

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene amewataka wawekezaji kufuata sheria za mazingira kabla ya kuanza uzalishaji.

“Sheria na kanuni zetu za mazingira zinawataka wawekezaji wa viwanda kupitia michakato kadhaa kabla ya kuanza uzalishaji.

“Wapo wawekezaji wanaopita njia za mkato na kuanza uzalishaji huku miundombinu ya msingi katika viwanda hivyo vikiwa bado havijakamilika hali inayosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi,”alisisitiza.

Waziri alisema hayo wakati wa ziara za kushtukiza katika maeneo ya viwanda ambapo alisema suala la kukagua ni ende- levu, ili kuhakikisha sheria na taratibu za kuhifadhi mazingira zinafuatwa na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini.

Akizungumza katika yake ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani hivi karibuni, Simbachawene alisema serikali inahamasisha na kuvutia uwekezaji katika viwanda kwa kuzingatia sheria na kanuni za utunzaji wa mazingira. “Kama Waziri mwenye dhamana ya mazingira nitaendelea kufanya ziara za kushtukiza sehemu mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa uwekezaji katika viwanda hauathiri mazingira au kuleta adha kwa wananchi sehemu husika,” alisema.

Alisema uwekezaji mzuri na endelevu ni ule unaojali na kulinda mazingira yanayozunguka, hivyo azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 itatekelezwa sambamba na utunzaji wa mazingira.

Kauli ya waziri ilikuja kutokana na ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha kuzalisha nondo cha Fujian Hexingwang kilichopo eneo la Kisemvule katika Wilaya ya Mkurunga, ambako wananchi walikuwa wakilalamikia kiwanda hicho kwa kutozingatia taratibu za utunzanji wa mazingira.

Simbachawene aliwaonya wawekezaji kuacha kutumia mwanya wa ujenzi wa viwanda kwa kukiuka sheria na kanuni za mazingira na kamwe wizara yake haitamvumilia mwekezaji wa aina hiyo.

Aidha, ametoa angalizo kwa viwanda ambavyo vinaendelea na uzalishaji huku vikiwa vimekamilisha taratibu na sheria za mazingira lakini wakati uzalishaji ukiendelea viwanda hukiuka taratibu zinazowangoza.

“Kuna viwanda vimefuata taratibu zote kupitia NEMC lakini wanapoanza uzalishaji hujikuta wanakiuka taratibu hizo, Ofisi yangu kwa kushirikiana na NEMC tutahakikisha tunapitia viwanda hivyo na kama vitabainika kuwa na makosa basi vitapigwa faini kwa mujibu wa sheria,”alisema.

Simbachawene ameyataja makosa ambayo yamekuwa yakijirudia kwa viwanda vingi ni pamoja na kutiririsha maji taka bila kuyatibu, mfumo mbovu wa utupaji taka za viwandani,hewa chafu na milipuko hali inayochangia uchafuzi wa mazingira na kuleta athari za kiafya kwa wananchi.

“Tunajenga uchumi wa viwanda ambao utaleta uwiano mzuri na ustawi wa jamii, tunawapongeza wale wote ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa kanuni na sheria za mazingira, lakini kwa wale ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu basi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,”alisema.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mkuranga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi