loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi vyuo vikuu nchini waadhimisha mwaka wa kichina

TAASISI ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuadhimisha mwaka mpya wa kichina umeandaa mashindano ya nyimbo kwa kutumia lugha hiyo kwa wanafunzi waliopo katika vyuo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kuboresha lugha hiyo.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Profesa Lin Yan katika mashindano hayo alisema anaamini wanafunzi kwa kupitia nyimbo wanaweza kujifunza kwa urahisi zaidi lugha hiyo.

Alisema katika mashindano hayo wanafunzi waliimba nyimbo za mahusiano, maisha pamoja na nyimbo mbalimbali za kufikirisha katika maeneo mbalimbali.

Alisema katika mashindano hayo vyuo 10 nchini vilishiriki kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Iringa. Alisema katika mashindano hayo washindi watatu watapata zawadi mbalimbali.

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi