loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha Setien alikuwa akiiota Barca kitambo

QUIQUE Setien anasema kuwa hawezi kufi kiria jinsi alivyokuwa akiota kwa muda mrefu nafasi ya ukocha wa Barcelona.

Kocha huyo wazamani wa Real Betis, jumatatu alitangazwa kuwa kocha wa Barca kufuatia kutupiwa virago kwa mtangulizi wake, Ernesto Valverde. Setien, 61, ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu, aliiongoza Betis kumaliza katika nafasi yao ya juu kabisa kuwahi kuifikia tangu mwaka 2005 na kucheza nusu fainali ya Kombe la Copa del Rey kabla ya kuondoka Mei.

“Kwa kweli napenda kuishukuru taasisi hii kwa kunipatia nafasi, “alisema kocha huyo Mhispania katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na timu hiyo.

“Hata sio katika ndoto zangu, hilo sikuwahi kulifikiria kama zinaweza kutimia. Napenda kuishukuru klabu. Nimefurahishwa na mradi huu pamoja na changamoto nitakazokutana nazo.”

Kocha huyo aliongeza: “Jana, nilikuwa natembea mjini kwetu na nilikuwa nakutana na ng’ombe, lakini sasa niko hapa Barcelona nawafundisha wachezaji bora duniani.”

Baada ya kuziongoza timu ndogo katika ligi, Setien aliiongoza Las Palmas hadi katika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, ikiwa ni nafasi yao bora kabisa kuwahi kuifikia katika kipindi cha miaka 40 na kufurahia mafanikio zaidi akiwa Betis. Katika msimu wa kwanza na Betis aliiongoza timu hiyo hadi katika nafasi ya sita na kufuzu kwa mashindano ya Ligi ya Ulaya.

Betis pia ilipata ushindi dhidi ya Barca, Real Madrid na Atletico Madrid wakati wa kipindi chake cha miaka miwili cha kuifundisha timu hiyo, na aliondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano katika kipindi cha majira ya joto. Barcelona kwa sasa inashika uongozi wa La Liga kwa tofauti ya mabao na imeshinda mataji manne kati ya matano yaliyopita.

“Namshukuru Ernesto Valverde kwa kuniachia kikosi kikiwa kileleni katika msimamo wa ligi, “alisema. “Lengo langu ni kushinda kila kitu! Unaweza kushinda kila kitu, hii ni klabu haina njia nyingine ya kufuata.

“Mwaka baada ya mwaka, kushinda mataji mengi iwezekanavyo. Nafikiri njia nzuri kushinda ni kucheza soka zuri. Lakini huwa hilo halitokei mara zote, lakini sio kwa mara moja tu, lakini ni kuhakikisha linakuwa jambo la kawaida.”

Setien huko nyuma aliwahi kusema kuwa atalia endapo mshambuliaji wa Barca na Argentina Lionel Messi atastaafu kucheza soka.

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments