loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TTCL waongeza muda wa kutoa huduma usajili wa laini

ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla ya kuzimwa kwa simu, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limeongeza muda wa kutoa huduma tangu jana kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili usiku.

Aidha alisema huduma hizo zitatolewa kwa siku ya leo Jumamosi na Jumapili kwa muda huo bila kujali kuwa ni siku za mwisho wa wiki. Meneja Huduma kwa Mteja wa shirika hilo, Laibu Leonard alisema hayo alipokuwa akielezea ufumbuzi wa changamoto ya kimtandao iliyojitokeza katika shirika hilo wakati wa usajili.

Leonard alisema kilichoonekana ni kwamba wananchi wengi wanasubiri dakika za mwisho za usajili hivyo ongezeko la wateja linakuwa kubwa nchi nzima na wakati mwingine mtandao kuzidiwa.

“Tunaomba wateja wetu pale wanapokutana na tatizo warudi tuwahudumie kwani tumeongeza muda wa kazi kuanzia asubuhi hadi saa mbili usiku kwa siku hizi mbili zilizobakia,” alisema.

Kwa upande mwingine zikiwa zimebakia siku mbili kabla ya kuzimwa kwa simu ambazo hazijasajiiwa kwa alama za vidole, wananchi wameomba muda uongezwe kutokana na changamoto ya kimtandao inayojitokeza wakati wa usajili kwenye kampuni za simu.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wananchi wakiwa wanasubiri mtandao urudi katika Ofisi za TTCL, ili waweze kusajiliwa baada ya mtandao kutokuwepo kwa muda waliokuwepo hapo. Juzi wananchi jijini Dodoma waliomba serikali ifikirie kuongeza siku za usajili huo hadi mwisho wa mwezi, mwaka huu.

Pia wananchi hao walishauri badala ya usajili huo kutegemea Mamlaka ya Vitambulisho (Nida) pekee, uwigo upanuliwe ili usajili huo uruhusiwe kutumia pia vitambulisho vingine vilivyosajiliwa kwa alama za vidole kama leseni za biashara, vitambulisho vya kupiga kura na pasi za kusafiria.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba alisema wananchi ambao laini zao za simu zitazimwa keshokutwa Januari 20 mwaka huu, wanaweza kuendelea na usajili wa laini zao kwa alama za vidole pale tu watakapokuwa wamepata kitambulisho cha taifa na wanaweza ama kurudisha laini zao zitakazofungwa au kusajili laini mpya kwa kuwa usajili huo ni endelevu.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi