loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru Singida yaokoa milioni 18/-

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Singida imeokoa zaidi ya Sh Milioni 18.11 kutoka miradi mbalimbali ya maendeleo na ukusanyaji mapato kwenye minada katika kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka jana.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwisho kwa mwaka 2019, Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Singida, Mzalendo Widege alisema kuwa katika kipindi hicho jumla ya kesi nane zilifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashauri ya jinai.

Kesi hizo ni pamoja na Ofisa wa Kazi kutoka Idara ya Kazi mkoa wa Singida ambaye alishawishi raia wawili wa China a kumpatia Sh 3,000,000 ili asiwachukulie hatua kwa kosa la kufanya kazi nchini bila Kibali.

“Wakati mtumishi huyo wa umma anashitakiwa kwa kushawishi na kupokea kiasi hicho cha fedha, raia hao wa kigeni wanashitakiwa kwa kosa la kutoa rushwa,” alifafanua.

Alitaja washitakiwa wengine katika kipindi hicho kuwa ni Hakimu wa mahakamani ya mwanzo Mtinko wilayani Singida, askari mgambo mmoja kutoka kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo na Mkuu wa Shule ya Sekondari Seth Benjamin wilayani Mkalama.

Aidha, alisema kuwa katika kipindi hicho Taasisi hiyo ilifanya mikutano ya hadhara 86, semina 69 na kufikia vilabu 71 vya wapinga rushwa kwa ajili ya kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa.

Katika hatua nyingine, jana Taasisi hiyo iliwafikisha mahakamani mkuu wa shule ya sekondari Lighwa wilayani Ikungi, Joseph Kweka na mwalimu wa shule hiyo, Yasin Shelukindo kwa tuhuma ya kutumia vibaya madaraka yao na kuuza jina la mwanafunzi mmoja ambaye alifaulu mtihani wa kwenda sekondari kwa kumpa mwanafunzi mwingine nafasi hiyo.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi