loader
Picha

Yanga kujiuliza kwa Azam leo

NI vita kati ya Yanga na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga watautumia mchezo huo kujaribu kupoza machungu ya kudharirishwa vibaya na Kagera Sugar kwa kupigwa nyumbani 3-0.

Kipigo hicho kimeifanya Yanga kuzidi kuwa mbali na Simba, ambao juzi wenywe walishinda 2-1 dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Azam wenyewe wanaingia uwanjani wakiwa na ari kubwa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipulizi ya Iringa kwenye Uwanja wa Taifa.

Mfano kwa msimu uliopita Yanga walizoa poiti zote sita walipokutana, ambapo mzunguko wa kwanza Azam walikubali kichapo cha bao 2-1, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex kabla ya kufungwa tena 1-0 katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Uhuru.

Hadi sasa kwenye msimamo, Yanga wanashika nafasi ya nane wakiwa na pointi 25 wakishuka uwanjani mara 13 wakati Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 29 baada ya kucheza michezo 14.

Kufuatia mtanange huo, Kocha wa Yanga Luc Eymael alisema baada ya kupoteza mchezo uliopita alishagundua udhaifu wa kikosi hicho na kuahidi kuyafanyia kazi kuhakikisha kwenye mchezo wa leo wanapata ushndi.

“Tumepoteza lakini nimeshagundua madhaifu ya kikosi na nitafanyia kazi kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam nan i matatizo madogo madogo tu,” alisema Eymael.

Kwa upande wake kocha msaidi za Azam, Iddi Chehe alisema wamepania kuendeleza wimbi la ushindi kama walivyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Lipuli na kikosi chake kipo vizuri kuwakabili Yanga.

“Tunajua tunaenda kucheza na Yanga sisi tunejipanga kwa ushindani na malengo yetu ni kuzoa pointi tatu muhimu kuendeleza kasi yetu ya ushindi, ” alisema

RAIS Dk John Magufuli ameiagiza Ofisi ya Rais Utumishi na ...

foto
Mwandishi: Tuzo mapunda

Weka maoni yako

2 Comments

 • avatar
  Balakha Mapunda
  18/01/2020

  Nachoshangaa Yanga Tunae Kikos Kpana Sasa Tunafel Wapi

 • avatar
  Balakha Mapunda
  18/01/2020

  Nachoshangaa Yanga Tunae Kikos Kpana Sasa Tunafel Wapi Bench Kuweni Makin Aibu Tumechoka By Balakha Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi