loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi Rukwa kupiga kura kuwataja walimu wakware

MKOA wa Rukwa wanafanya mpango wa wanafunzi kupiga kura za siri ili kuwabaini walimu ‘wakware’ linatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa .

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo kwa kile alichodai kuongezeka kwa walimu wa kiume katika shule za msingi na sekondari kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao wa kike na kuwasababishia ujauzito.

“Walimu wa kiume mkoani Rukwa baadhi yao wamekengeuka wanakuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao na kuwapaa ujauzito… mpango wa wanafunzi kupiga kura za siri ili kuwabaini walimu wakware katika shule zao uko mbioni kuanza,” alisema .

Wangabo alisema; “ Yamekuwepo matukio ya walimu kadhaa wakiwemo walimu wakuu na wakuu wa shule kukamatwa na kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashataka ya kubaka na kuwapatia ujauzito wanafunzi… ila Mkuu wa Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi mwambao mwa Ziwa Tangayika, Kata ya Kala wilayani Nkasi ,( Eradi Kapyela) anayetuhumiwa kuwapatia wanafunzi wake watano ujauzito amefanikiwa kutoroka na inasemekana amekimbilia kujificha nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC),” alibainisha.

Aliongeza kuwa wilaya ya Nkasi ilifanya majaribio katika shule mojawapo ya sekondari na wanafunzi walipiga kura za siri na matokeo yake walimu wote wa kiume walibainika kuwa na mahusiano na wanafunzi wa kike .

“Kupitia mpango huo wa majaribio baadhi ya wanafunzi wa kike walivunja ukimya kwa kutoa taarifa ya mwanafunzi mwenzao wa kike ambaye alikuwa amewekwa kinyumba na mwalimu wake,” alibainisha na kuongeza kuwa mkoa wa Rukwa umedhamiria kutokomeza mimba za wanafunzi ifikapo 2025 kwa Kikao cha Ushauri Mkoa wa Rukwa (RCC) kupitisha rasimu ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni .

Wanganbo alisema takwimu za matukio ya mimba za utotoni katika mkoa wa Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka 2017 hadi 2019 ni matukio 722 yameripotiwa kati yao 171 walikuwa wakisoma katika shule za msingi na 551 walikuwa wanafunzi wa sekondari.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments