loader
Picha

Chungu ya NIDA usajili wa laini za simu

OFISA msajili wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa ( NIDA ) mkoani Shinyanga, Nathanael Njau amesema zimebaki siku mbili za usajili wa laini kwa alama za vidole lakini changamoto imejitokeza watu kutaka kujisajili siku hiyo hiyo na kudai wapatiwe namba kitu ambacho hakiwezekani.

Akizungumza na waandishi wa bahari jana kuhusu usajili wa vitambulisho vya taifa , alisema kwamba idadi kubwa iliendelea kujitokeza kwa mtindo huo ambapo amedai amekuwa akiwaeleza utaratibu wa ukishajiandikisha unatakiwa ukae kwa muda wa wiki mbili.

Njau alisema kuwa Rais Magufuli alitanganza usajili wa laini za simu ni mwisho tarehe 20, lakini tarehe za katikati watu walikuwa hawajitokezi wamekuwa wakijitokeza siku zikikaribia kuisha .

“Hawa wote mnaowaona kwenye foleni sio wote waliojisajili zamani bali wengine wamejisajili leo (jana) na jana (juzi) wamekuja hapa kutaka wapatiwe namba ili wakajisajili laini zao kwa alama za vidole utaratibu uliopo ukishajisajili unatakiwa ukae wiki mbili na mfumo uweze kusoma taarifa zilizotolewa na mhusika,” alisema.

Njau alisema kuwa mwezi Oktoba mwaka jana alikwenda maeneo ya vijijini kwa ajili ya wananchi kujisajili walijitokeza wengi na kupata vitambulisho na kuwa wanaodai wametoka mbali huenda walipokuwepo waandikishaji wa NIDA hawakuwepo au kujitokeza.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Rajabu Mtiula ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

2 Comments

 • avatar
  Sulemani zephania mlingwa
  19/01/2020

  Laini zifungwe ila uandikishaji uendelee mpaka vijijini

 • avatar
  gwagu
  21/01/2020

  Vungeni laini zote ambazo hazijasajiliwa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi