loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanafunzi afariki akitoa mimba

MWAFUNZI, Zawadi Pindua (15) aliyekuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Mwimbi iliyoko wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa amekufa baada kutoa mimba ili aendelee na masomo baada ya muhula wa masomo kuanza Januari mwaka huu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Justine Masonje amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwanaume aliyempa ujauzito na kumsaidia mwanafunzi huyo kutoa mimba iliyomsababishia umauti amekamatwa .

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji ha Tunyi kilichopo katika kata ya Mambwe Nkoswe wilayani Kalambo Januari 13 mwaka huu saa tisa mchana nyumbani kwa mwanaume anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Kamanda Masonje alieleza kuwa Ofisa wa Kijiji cha Tunyi Hassan Lupasa aligundua mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa nyumbani kwa mtuhumiwa na aliongoza msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa .

“Marehemu na mtuhumiwa waliondoka kijijini Mwimbi Januari 22, mwaka huu na kwenda kujificha katika kijiji cha jirani cha Tunyi ambapo mtuhumiwa alimsaidia mwanafunzi huyo kutoa mimba ili shule zikifunguliwa Januari mwaka huu arudi shule na kuendelea na masomo yake,” alieleza.

Kamanda Masonje aliongeza kusema kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali wa shauri lake kukamilika .

foto
Mwandishi: Petty Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi