loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzanite kuivaa Uganda Kombe la Dunia

TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, ‘Tanzanite’ leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kusaka ushindi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uganda.

Mchezo huo wa kwanza Tanzanite inahitaji matokeo mazuri kuhakikisha inajiweka pazuri kabla ya kwenda kurudiana nao ugenini baadae nchini Uganda.

Kocha wa Tanzanite, Bakari Shime amewatoa hofu Watanzania kwa kujinadi kuwa ana hazina kubwa ya wachezaji wenye uzoefu hivyo ana imani watafanya vizuri.

“Maandalizi yetu ni ya muda mrefu, tuna wachezaji wengi na tulikuwa kambini pamoja na wachezaji wa timu ya umri wa miaka 17 na tunaruhusiwa kuwatumia hivyo tunategemea mambo yatakuwa mazuri,” alisema Shime.

Shime alisema amewaandaa wachezaji kufanya vizuri sio tu katika uwanja huo wa nyumbani bali hata watakapokwenda ugenini.

Alisema anaijua Uganda ni moja ya timu nzuri ukanda huu wa Afrika Mashariki hivyo, amejipanga kimbinu dhidi yao ili kupata matokeo mazuri.

Kocha huyo alisema mapungufu aliyaona katika mchezo wa timu ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 aliyafanyia kazi kwa vile baadhi ya wachezaji wapo katika kikosi hicho cha Tanzanite.

Viingilio vya mchezo huo utakaochezwa saa 10:00 jioni ni Sh 5,000 kwa VIP A na Sh 1,000 kwa VIP B huku mzunguko ikiwa bure.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi