loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Laini za simu kuzimwa kwa awamu

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itazima kwa awamu laini za simu, ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole na katika kutekeleza jukumu hilo, watatumia ustaarabu na utalaamu.

Lengo la kutumia ustaarabu na utaalamu katika hilo ni kuwafanya wamiliki wa laini hizo, kurudi kuhuisha laini zao. Lakini, pia kuifanya mifumo ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) isizidiwe, endapo laini nyingi zitafungwa kwa wakati mmoja.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba katika taarifa yake aliyoitoa kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1).

Kilaba amesema jumla ya watu 975,000 ambao tayari wana vitambulisho vya taifa na hawajasajili laini zao kwa alama za vidole, ndiyo waliokuwa kwenye kundi la kuzimiwa laini zao tangu juzi saa 6:00 usiku.

“Kwa hiyo tunaanza kuzima laini leo (juzi), na hatma ya wale ambao hawajasajili laini zao iko katika makundi mbalimbali, kundi la kwanza ni wale wenye namba za utambulisho wa kitaifa ambao idadi yao ni 656,091, hawa wako tayari kuzimiwa leo(juzi),”amesema Kilaba.

Kundi jingine alilolitaja ni la wale ambao walisajili laini zao mwanzoni kwa kutumia kitambulisho cha taifa, lakini siyo kwa alama za vidole ambao idadi yao ni 318,950.

Amesema watu hao walitakiwa kurudi kuhuisha usajili wao kwa alama za vidole, lakini hawakufanya hivyo, nao laini zao zilizimwa. Alisema laini ambazo hazijakamilisha usajili, zitazimwa kidogo kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, kwa sababu hawawezi kuzima laini milioni tano au milioni kumi kwa mara moja, kwa kuwa mifumo ya NIDA haitaweza kuhimili kuhudumia idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja.

“Tunahitaji watu hawa warudi, tukiwazimia tunatarajia kesho warudi kwenye foleni za kuhuisha laini zao, wakienda wengi zaidi hawatapata huduma kama walivyojaa katika siku tatu za mwisho mpaka mifumo ya NIDA ikaelemewa, kwa hiyo tunaenda kiustaarabu na kiutalaamu,”alieleza Kilaba.

Kwa mujibu wa Kilaba, maendeleo katika sekta ya mawasiliano yamesababisha watu wengi kuwa watumiaji wa laini za simu za mkononi, jambo ambalo licha ya kuwa zuri lakini pia limekuwa na changamoto.

Alitaja changamoto hizo zilizosababishwa na matumizi ya laini za simu kuwa ni matatizo ya kiusalama, undanganyifu na wizi.

Alisema kutokana na matatizo hayo, yaliyosababishwa na matumizi ya laini za simu, ndipo serikali ikaamua laini zote zisajaliwe upya kwa kutumia kitambulisho cha taifa na alama za vidole ili kumjua kila mtumiaji wa laini ya simu.

Laini kusitishiwa huduma Kilaba alisema lengo la TCRA siyo kumnyang’anya mtu laini yake, ambayo ameizoea na kuipenda, ila itakachokifanya ni kuisitisha kutoa huduma na kupokea huduma ili mmiliki aihuishe.

Alisema laini ambazo zimesitishwa kutoa huduma, zitaweza kupokea ujumbe mfupi pekee, utakaokuwa unamweleza mhusika hatua za usajili wake, lakini haitaweza kufanya vitu vingine ikiwemo huduma za data, kutuma na kupokea fedha hadi hapo usajili wake utakapokamilika.

Awageukia wananchi Kilaba alisema tabia ya kuchelewa kutekeleza maagizo ya serikali kunakofanywa na wananchi, kunarudisha nyuma maendeleo hususani katika mambo mazito na ya msingi ya kitaifa, ambayo yanahusu hata usalama wao wenyewe.

Alisema japo TCRA ilipanga kuzima laini hizo Desemba 31 mwaka jana, lakini kwa upendo na huruma ilipofika Desemba 27, Rais Dk John Magufuli aliamua kuongeza siku 20 ili wananchi wakamilishe usajili wa laini zao. Lakini, cha kusikitisha wananchi walipungua kwa kiasi kikubwa na waliendelea kupungua na kufanya usajili kushuka chini.

Wananchi wazungumza Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili jana, walisema wanapata mawasiliano kama kawaida, licha ya laini zao kutosajiliwa kwa alama za vidole na hawana Namba ya Utambulisho ya NIDA.

“Mimi namba yangu sijasajili na wala sina namba ya utambulisho, lakini tangu asubuhi nawasiliana na jamaa zangu kama kawaida, mpaka sasa nimeshawasiliana na watu wanne kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na data pia natumia, laini ninayotumia

ambao wengine wanatumia mitandao ya Airtel kama yeye na wengine wanatumia Tigo na Vodacom. Mkoani Tanga, baadhi ya mawakala wa usajili wa mitandao ya simu, walitumia fursa hiyo kujitengenezea pesa, kwa kuwatoza fedha wateja ambao hawajasajili laini na ambao hadi juzi wamenusurika kuzimiwa.

Gazeti hili baada ya kupata taarifa hizo, liliamua kufanya uchunguzi katika mitaa mbalimbali, ambapo mawakala hao sasa wamekuwa na maringo, tofauti na awali ambapo walikuwa wakizunguka mitaani kutafuta wateja kuwafanyia usajili kwa gharama ya Sh 1,000, lakini ukienda ofisini ilikuwa ni bure.

Lakini jana hali ilikuwa ni tofauti, ambapo wote wamebadilika na mawazo yao ni kulifanya zoezi hilo la kutengeneza fedha.

Mwandishi alikwenda mitaa ya Barabara 12 (stendi ya Daladala) na laini ya Halotel kwa wakala aliyefunga mwamvuli na kujifanya anataka kusajili laini ya Halotel, alipokewa kwa shangwe na baada ya kuuliza gharama, aliambiwa atoe Sh 1,000 kwa usajili wa laini moja. Imeandikwa na Cheji Bakari Tanga

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi