loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ni Yanga Vs Singida United leo

BAADA ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika uwanja wa nyumbani, Yanga imepania kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United katika mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Liti (zamani Namfua) Singida.

Mchezo huo ni mtihani mwingine kwa kocha Luc Eymael na kufufua matumaini ya kuwania ubingwa na kuwafuta machozi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuanza kibarua chake vibaya akifungwa na Kagera Sugar na Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote, kwani Singida United watahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kutoka kwenye nafasi za kushuka daraja kwenye msimamo wa ligi.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25 wanakutana na Singida ambayo imetoka kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0, lakini inashika nafasi ya 19 wakiwa na pointi 10 baada ya kucheza michezo 16.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na historia Yanga kutoshinda mchezo wa ligi katika uwanja huo tangu Singida United ipande ligi kuu, rekodi za msimu uliopita zilipokutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoka suluhu.

Soka lina matokeo ya ajabu, timu iliyojiandaa kisaikolijia na kiufundi ina uwezo wa kupata pointi tatu ambazo zinaweza kusaidia kusogea hatua nyingine kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo mwingine leo, Azam FC watamenyana na Mwadui FC mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga. Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 katika michezo 15 sawa na Mwadui inayoshika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 17 .

Mchezo huo ni mgumu kulingana na rekodi za msimu uliopita kwani walipokutana kwenye uwanja huo walitoka sare ya kufungana bao 1-1 ingawa mechi ya mzunguko wa pili Azam FC walishinda 1-0 katika uwanja wa Azam Complex.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi