loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Baraza la Kilimo lahadharisha utumiaji vyakula kutoka nje

BARAZA la Taifa la Kilimo Tanzania limesema vyakula katika masoko vinavyoliwa nchini vinatakiwa kuangaliwa viwango na ubora wake kwa kupimwa kama vinavyofanywa vinavyosafi rishwa nje ya nchi.

Hatua hiyo inatokana na kuwa utafiti uliofanywa nchini na baraza hilo umebaini katika masoko ya ndani vyakula vingi vina sumu kutokana na kulimwa kwa kutumia viuatilifu vyenye sumu ba pia kutofuata viwango stahiki vya taifa.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jackline Mukindi alipokuwa akifungua Maonesho ya Wakulima wa Bidhaa za Klimo yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi na kuhudhuriwa na wadau wa ndani na nje zaidi ya 12,000,yaliyoandaliwa na shirika la FROLESTA.

Alisema vyakula vinavyosafirishwa kimataifa viwango vyake vinaangaliwa kwa umakini sana tofauti na vile vinavyouzwa ndani ya nchi hivyo wataweka mkakati wa vyakula vya ndani kupimwa kwa viwango stahili.

Alisema kutokana na kuuzwa kwa vyakula vya sumu, magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari na saratani yameongezeka sana hivyo ni vema kuhamasisha kilimo kisichotumia kemikali.

Mukindi alisema ili kukabiliana na bidhaa zenye sumu walaji wanatakiwa kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini ili kulinda afya zao kwani kumekuwa na tabia za walaji hususani katika hoteli kubwa kupenda bidhaa toka nje ya nchi.

Alisema utafiti uliofanywa katika sekta ya madini katika ilaji ilibaini asilimia 65 ya bidhaa za mboga na matunda zinaingizwa toka Afrika Kusini wakati bidhaa hizo zinapatikana nchini.

Alitaka wakulima kulima kwa kuangalia fursa za biashara kimataifa na kikanda kwani miaka mitano ijayo watakaotengeneza fedha ni wanaolima kibiashara hususan katika kilimo cha mbogamboga na matunda.

Mwenyekiti huyo wa baraza alisema sekta hiyo inakua kwa kasi nchini kutokana na kuwa kilimo kinakua kwa asilimia 3.5 kwa mwaka lakini katika mbogamboga na matunda inakua kwa asilimia 11 hadi 12 huku awali walikuwa wakiuza mazao ya dola milioni 64 lakini sasa fursa yake ni dola milioni 700 huku Tanzania ina fursa ya kufanya biashara ya mazao hayo ya dola bilioni sita.

Naye, Rais wa Shirika la Kuendeleza Kilimo hai Afrika na Tanzania (TOAM), Jordan Gama alibainisha kuwa kilimo hai kimekuwa na maendeleo kwa kupata fursa nyingi ndani na nje ya nchi huku wizara ya kilimo ikiweka kilimo hai katika sera ya maendeleo ya kilimo.

Alisema pia wizara ikianzisha kitengo ambacho baadaye kitakuwa kurugenzi huku vyuo vikuu vikianza kutoa mafunzo ya kilimo hai huku kukiwa na tafiti za teknolojia mbalimbali katika kukabiliana na visumbufu vya mazao.

Alisema mkoani kilimanjaro vikundi saba vimethibitishwa baada ya kukidhi viwango kuuza kahawa nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa FROLESTA, Richard Mhina alisema shirika hilo limefanikiwa kuanzisha vikundi 450 katika mkoa wa Kilimanjaro na kuchangia uhifadhi wa mazingira ikiwemo kuhakikisha barafu katika Mlima Kilimanjaro haipokei usalama wa chakula nakuchangia kukua kwa uchumi wa wanavikundi.

Pia wakulima wamekuwa wanatambua masoko ya ndani na nje kwa kuhakikisha wanawapatia elimu stahili katika ujasiliamali na ukulima wa mazao ya aina mbalimbali kwa kutumia kilimo kisicho na kemikali.

Naye, mwakilishi wa vikundi 17 vinavyohitimu mafunzo, toka shirika la Frolesta, Mwinjilisti Saimoni Tumaini alisema vikundi hivyo vinatoka Shengenya, sashari, Hai na Moshi Vijijini ambao wamepata mafanikio kwa kutunza mazingira katika vyanzo vya maji, pamoja na mafunzo.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments