loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC aagiza tathmini ya maafa mvua zinazoendelea

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametaka wilaya zote mkoani hapa kufanya tathimini ya maafa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Pia ametaka kufanyika utaratibu wa kuhamisha wakazi wanaoishi kwenye bonde la mpunga wilayani Bahi, ambao wengi nyumba zao zimebomoka.

Aliahidi kutoa Sh milioni tatu kwa ajili ya kununulia chakula kwa wakazi walioathirika na mafuriko huku, Ofisa maafa wa wilaya, Hamisi Mfuko akisema tani 30 za chakula zinahitajika ili kuwasaidia wananchi waweze kuendelea na shughuli za kilimo.

Akikagua athari za mafuriko katika wilaya ya Bahi alisema: “Mvua zinatufundisha kuna uharibifu mkubwa wa mazingira, ujenzi wa nyumba lazima uzingatie viwango bora na wakati huo huko kuhakikisha mazingira yanatunzwa.”

Pia alitaka kila halmashauri mwaka huu kuingiza mpango wa uvunaji wa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa ya maji. “Kwenye Kata zenye changamoto ya mafuriko kama kata ya Chali lijengwe bwawa kwenye sehemu maji yanapotuama sana,” alisema.

Akizungumza kwenye eneo la bonde ambapo wananchi wamejenga huku shughuli za kilimo cha mpunga zikindelea aliwataka wananchi hao kuondoka maeno hayo ambayo si salama kwao.

Kwenye eneo hilo ambalo nyumba nyingi zimebomoka , njia zote zimejaa maji, baadhi ya wakazi wake wanaishi kwenye mahema yaliyotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye nyumba yake imebomoka huku nyingine ikiwa katika hali mbaya ya kutaka kuanguka, Faustila Daud alisema mvua nyingi zinazoendelea kunyesha zimebomoa makazi mengi katika kitongoji hicho cha Mji mpya.

Mkazi huyo alisema yeye pamoja na watoto wake wamekuwa wakilala kwenye hema na nyumba hiyo wanaitumia mchana kwa ajili ya kupikia tu. Mussa Nyagalu ambaye alikutwa akipandikiza mpunga alisema hali ya makazi ni mbaya na hata yeye nyumba yake imenguka.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi