loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

200 wanufaika na huduma za kliniki tembezi BMH

ZAIDI ya wakazi 200 wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara wamenufaika na huduma ya matibabu ya kliniki tembezi iliyotolewa kwa siku tatu wa wataalamu wa kibingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Huduma hizo zilitolewa kuanzia Januari 16 hadi 18 mwaka huu wilayani humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini hapa na kitengo cha mawasiliano, huduma ya kliniki tembezi ilijumuisha utoaji wa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya moyo, figo na mfumo wa mkojo na upasuaji.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Dk Paschal Mbota alitoa shukrani kwa madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa kumesaidia watu wetu ambao walikuwa wakikosa huduma za kibingwa kama hizi.”

Dk Mbota alifahamisha zaidi kuwa mpango huo pia umesaidia Hospitali ya Wilaya kuongeza mapato ndani kwa siku tatu za huduma, na kusisitiza haja ya kujenga ushirikiano wa kudumu katika utoaji huduma kati ya BMH na Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

Alisema kuwa muda wa siku tatu wa kutoa huduma za kibingwa za kliniki tembezi haukutosha kwa sababu ya kuwapo idadi kubwa ya watu ambao walijitokeza kufuata huduma za kibingwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Dk Geko Jackson alisema madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto wamefaidika sana na utaalamu wa madaktari bingwa wazoefu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Naye Sufiani Rajabu (83), mkazi wa eneo la Kibaya Kati huko Kiteto, ambaye alifanywa upasuaji wa njia ya mkojo wakati wa utoaji huduma ya kliniki tembezi alisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa takribani miezi tisa.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments