loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rehema Nchimbi walalamikia majitaka

WAFANYABIASHARA wa Soko la Rehema Nchimbi Jijini hapa wamelalamikia chemba za majitaka zinazotiririsha maji na kuingia katika maeneo wanayofanyia biashara. Wamesema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao na za wateja hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao walisema chemba hizo zimekuwa zikifumuka na kuleta adha na wakati mwingine kupelekea wao kushindwa kufungua ofisi zao.

Mmoja wa wafanyabiashara wa kuuza chakula, Amina Tawaka alisema wamekuwa wakipata adha kubwa pindi chemba hizo zinapofumuka na kisha maji yenye uchafu kutuama kwenye maeneo yao ya biashara.

Alisema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara na linahitaji kushughulikiwa ili kumaliza kero hiyo. Wakati huo huo, wafanyabiashara hao wameziomba mamlaka husika kwenda kuangalia na kuona kwamba ni kitu gani ambacho kinaendelea sokoni hapo.

Mfanyabiashara mwingine, Mena Chacha alitaka pia kuangaliwa kwa vibanda ambavyo havijamalizika kujengwa ambapo wahusika hawachukui hatua yoyote na kufanya baadhi ya vibanda hivyo kutumika kama vyoo, hali ambayo haipendezi.

Kwa upande wake, Katibu wa Soko la Rehema Nchimbi, Peter Mboya alisema kwa kawaida chemba zinapoziba huwa wanawataarifu uongozi wa Dodoma Canival na Kimbinyiko ambao ndio watumiaji na hufika na kulitatua.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi