loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stamico kuanzisha mradi wa kusafisha dhahabu

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) lipo katika hatua za awali za kuanzisha mradi wa kusafi sha dhahabu na tayari kampuni ya ubia ya Mwanza Precious Metals Refi nery imeanzishwa.

Hayo yamebainishwa juzi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa (STAMICO) Dk Venance Mwase wakati akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini taarifa kuhusu utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za maendeleo ya shirika hilo kwa kipindi cha nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa niaba ya Waziri wa Madini.

Dk Venance ameieleza kamati hiyo kuwa mradi huo utaendeshwa kwa ubia ambapo Stamico itakuwa na hisa asilimia 25 na mwekezaji asilimia 75, huku ikilelezwa kwamba mradi huo utakaojengwa jijini Mwanza utahusisha kujenga mtambo wenye uwezo wa kusafisha wastani wa kilo 200 hadi 500 kwa siku.

Aliongeza kuwa makadirio ya fedha zinazohitajika ni dola za Marekani milioni 58.204 ambazo zimepangwa kwa ajili ya ununuzi wa mtambo wa kusafishia dhahabu.

Pia gharama za awali za mradi, kununua dhahabu kutoka katika masoko pamoja na gharama za uendeshaji.

Aidha, Dk. Mwase alisema katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2019, tayari mradi umetekeleza majukumu kadhaa ikiwemo kupata leseni ya kujenga na kuendesha mtambo huo, kusainiwa mkataba wa ubia pamoja na kuanza taratibu za uanzishwaji wa kampuni ya ubia na kupata eneo la ujenzi wa mtambo chini ya Ukanda wa Maeneo Huru ya Kiuchumi(EPZA).

Kuhusu Mgodi wa Stamigold ambao ni Kampuni tanzu ya shirika hilo, alieleza kamati hiyo kuwa kuanzia Julai hadi Desemba, 2019, mgodi huo umezalisha na kuuza wakia 7,133 za madini ya dhahabu na wakia 879.19 za madini ya fedha, vyote vikiwa na thamani ya Sh 24,172,700,255.34.

Kuhusu mradi wa makaa ya mawe katika Mradi wa Kabulo na Kiwira, alisema jumla ya tani 4,359.10 ziliuzwa na kulipatia shirika Sh 17,558,184.76 na kuongeza kuwa, “shirika lilifanikiwa kulipa mrabaha, ada ya ukaguzi na tozo ya halmashauri ya Sh 23,645,000.62.

Aidha aliongeza kuwa mgodi umeendelea kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 400.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akitoa ufafanuzi wa hoja zilizoibuliwa na kamati, amewatoa hofu wajumbe wa kamati hiyo kuhusu maendeleo ya Stamico ambapo ameeleza pamoja na changamoto zinazolikabili, linakua na linafanya vizuri.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi