loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tahadhari ya TMA ipewe uzito

TAHADHARI iliyotolewa juzi na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya kuwepo kwa mvua kubwa katika mikoa minne, hainabudi kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TMA, mvua ilianza jana ambapo katika mikoa tajwa, mvua hiyo ilinyesha hata kama si kwa kiwango kikubwa lakini pia iliambatana na upepo mkali.

Taarifa hiyo ilibainisha kwamba mbali na mvua na upepo, pia kuna mawimbi katika maeneo ya bahari kwa kipindi cha siku nne. TMA walitaja mikoa saba, ikiwemo Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro na Tanga.

Maeneo ya mikoa ambayo mbali na mvua pia itakumbwa na upepo mkali na mawimbi ni Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.

Kwa kuwa mikoa hiyo imetajwa, ni ushauri wetu kwamba, wakuu wa mikoa, wilaya pamoja wakurugenzi wa halmashauri katika wilaya hizo wakishirikiana na viongozi wengine, wachukue hatua kwa kuhamasisha watu wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kupata maeneo kwa ajili ya kujihifadhi.

Waswahili wanasema ni heri ya kinga kuliko tiba, ina maana kubwa katika kukabiliana na majanga ambayo tayari yanaweza kunuswa kupitia utabiri wa hali ya hewa.

TMA ilisema mvua kubwa iliyoanza jana ingeendelea hadi Jumamosi kesho. Ikizungumzia athari zinazoweza kujitokeza, TMA ilisema katika mikoa inayotarajiwa kuwa na mvua kubwa kutakuwa na uharibifu wa miundombinu na mali katika baadhi ya maeneo, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Tunaungana na TMA katika kuwakumbusha wakazi katika maeneo tajwa kwamba hivi karibuni mvua kubwa ilinyesha kwa takribani saa saba mfululizo jijini Dar es Salaam, ilisababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Wananchi walitumia muda mrefu kufika kwenye shughuli zao za kila siku. Wengine walipata hasara kwa nyumba na samani zao, kuharibika kwa maji.

Mabasi ya mwendokasi yalisitisha shughuli zake kutokana na barabara kufurika maji katika eneo la Jangwani. Ni kotokana na adha tulizoziona, tunaamini, tahadhari ya TMA itachukuliw akwa uzito mkubwa ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kuepukika.

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), Jumanne ya wiki hii lilizindua ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi