loader
Magufuli- Kama hutaki kufuatwa ondoka

Magufuli- Kama hutaki kufuatwa ondoka

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John Magufuli amesema, kama kuna kiongozi serikalini hataki kufuatwa fuatwa na watendaji wa chama hicho aondoke.

Ametoa msimamo huo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na viongozi wa chama hicho na jumuiya zake ngazi ya wilaya na mkoa kwenye mikoa yote 32.

Ameagiza viongozi hao wahakikishe miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwamba atasikitika sana ikitekelezwa chini ya kiwango wakati viongozi hao wapo.

“Msikae kimya mnapoona miradi ya Serikali inadorora. Waelezezi viongozi wa Serikali kwenye wilaya na mikoa husika na mkiona hatua hazichukuliwi mjulisheni hata Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Ninyi ndio watawala. Tulizunguka kufanya kampeni ili tutawale…jeuri ya kutawala ni kutawala kweli, anayekuja pale ni mtumishi, wewe ni mtawala ilimradi tu usivuke nje ya mipaka ya sheria za nchi” amesema Dk Magufuli.

Amesema chama lazima kiangalie matokeo ya utekelezaji wa miradi na kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM lazima lazima viongozi wote walioteuliwa watambue kuwa wanatekeleza Ilani ya chama hicho.

“Wala pasitokee kiongozi yeyote ndani ya Serikali anayesema chama kinanifuata fuata. Lazima chama kikufuate fuate, kama hutaki kufuatwa fuatwa na chama ondoka upishe tuweke watu wengine. Chama ndio waajiri, chama wanataka kuangalia Ilani ya Uchaguzi inatekelezwaje”amesema Magufuli.

Amewataka viongozi hao wa chama waitetee Serikali na kutangaza mafanikio na kwamba kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/dd1d987a6f742f3a4e4806ccdd9706bd.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi