loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli aruhusu makinikia yauzwe

RAIS wa Tanzania Dk John Magufuli ameruhusu makontena yenye makinikia yaliyokamatwa bandarini Dar es Salaam yauzwe.

Ameagiza yakabidhiwe kampuni ya Twiga Minerals Corporation, atafutwe mteja yauzwe ili Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wanufaike.

Ametoa ruhusa hiyo leo Ikulu, Dar es Salaam baada ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick kusaini mikataba tisa ya makubaliano yakiwa ni matunda ya mazungumzo yaliyoanza mwaka 2017.

Kwenye tukio hilo lililohudhuriwa pia na viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais amesema, kusainiwa kwa mkataba kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick ni ushindi mkubwa na anamshukuru Mungu kwa hilo.

“Na hicho ndicho tulichokuwa tunakitaka, kwa hiyo makubaliano haya yamemaliza tag of war kati ya pande zote mbili. Na kuanzishwa kwa kampuni hii ya Twiga sasa nataka kuwahakikishia katika pande zote mbili mnaoendesha kampuni yale makontena ambayo yako bandarini ambayo tuliyashika sasa mkatafute wabia vizuri muuze kwa faida ya kampuni ya Twiga”amesema Rais Magufuli.

Rais amesema kusainiwa huko ni mwanzo wa ukurasa mpya msafi sana na maisha mapya na amezitaka pande mbili zinazomiliki kampuni ya Twiga zisimamie utekelezaji wa makubaliano hayo.

Ameihakikishia kampuni ya Barrick na wawekezaji wengine duniani kuwa kuwa Tanzania ni eneo bora zaidi kwa uwekezaji hasa ikizingatiwa kuwa ni nchi tajiri.

“Na ndugu zetu Barrick I can guarantee you now the game is over (nawahakikishia tatizo limekwisha), chapeni kazi, kafanyeni kazi kwa sababu ninyi Barrick mna expertise (utaalamu), mna capital (mtaji), sisi we have the raw materials (tuna malighafi). Dhahabu iliwekwa Tanzania, haikuwekwa kwingine, aliyeiweka Tanzania ana makusudi nayo”amesema Rais Magufuli.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments