loader
Picha

Ndugai kuzindua kadi Simba

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai anatajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kadi ya Simba itakayo kuwa maalumu kwa wanachama na mshabiki kwa ajili ya kuichangia fedha za kujiendesha kimaendeleo.

Kadi hiyo ya kibenki imeanzishwa na timu hiyo kwa kushirikiana na Benki ya Equity, ambazo zinawataka wapenzi na mshabiki wa timu kuchukua kadi hizo ili kuisapoti maendeleo ya timu kwa kumiliki hisa.

Akizungumza Dar es Salaam na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema Spika Ndugai atazindua kadi hizo rasmi kwa mshabiki wa Simba Kanda ya Kati Januari 29 jijini Dodoma.

Alisema baada ya hapo Spika atazindua tawi la kisasa la Simba ndani ya bunge hilo litakalo itwa Simba Mjengoni, ambapo mashabiki wote wa klabu hiyo ambao ni Wabunge watapewa kadi.

“Ili uwe mwanachama halali lazima umiliki hisa ndani ya Simba na tumemuomba Spika Ndugai kutuzindulia kadi zetu Makao Makuu ya Bunge, Dodoma ili kuhakikisha mpango wetu unakamilika kama tulivyopanga,”alisema Manara.

Alisema wakimaliza zoezi la kuandikisha wanachama wa Kanda ya Kati zoezi hilo litahamia mkoani Morogoro, lengo likiwa ni kuhakikisha wanawafikisha wanachama na mashabiki wa nchi nzima. Alisema ili wanachama na mashabiki wafanikiwe kupata kadi hiyo, lazima wahakikishe wanakuwa na kadi ya kutoka NIDA au ya Kupiga Kura

TIMU za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi