loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kituo kuendeleza kilimo hai Tanzania

KITUO cha kujifunza kilimo hai cha Mtakatifu Joseph (SJS) kilichopo Mwanga mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Same kimedhamiriwa kuendeleza kilimo hai nchini kwa kutoa mafunzo kuhusu kilimo hicho kwa kutumia teknolojia mbalimbali rafi ki wa mazingira .

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kuona jinsi wanavyozalisha mazao, mifugo pamoja na utoaji tiba mbalimbali kwa kutumia mimea ya asili, Mkuu wa kituo hicho, Padre Alwyn de Souza alisema shamba hilo lilianza mwaka 2017.

Alibainisha kuwa walianza kilimo hicho katika wilaya hiyo, baada ya Askofu wa jimbo hilo Logath Swai kutembelea India na kuona jisi wanavyolima mazao mbalimbali kwa kutumia kemikali za kukuza na kuondoa wadudu kutokana na teknolojia za vitu vya asili.

Padre De Souza alisema baada ya Askofu kuvutiwa na kilimo hicho cha asili ,yeye aliteuliwa kufika na kuanza kulima huku akisaidiwa na Mkuu wa Shamba hilo Martini Muhando na wafanyakazi wengine.

Alisema lengo ni kuhakikisha wanakuwa na upendo kwa watu kwa vitendo kwa kuhakikisha teknolojia wanazotumia wanaelekeza kwa wananchi wengine hususan katika vijiji vya jirani na eneo hilo na vikundi mbalimbali kutoka maeneo mengine.

“Tumedhamiria ,kuhakikisha kituo hiki kinakuwa chuo maalumu kwa ajili ya mafunzo ya kilimo hai nchini kwa watu kujifunza kwa vitendo kuhusu kilimo hai ili kulinda afya ya Watanzania na kilimo endelevu,” alisema.

Padre De Souza alisema kituo hicho kimedhamiria kuwafundisha watanzania ambao ni wakulima kwa asilimia takribani 70 kuvua samaki na siyo kuwapa samaki kwa kuwafundisha matumizi ya teknolojia hizo asili ili waweze kutumia katika maeneo mengi nchini.

Akizungumzia baadhi shughuli katika shamba hilo, Mhando alisema mbali na kulima mazao ya aina mbalimbali ikiwemo mihogo, viazi mbogamboga ,matikiti maji,matango,nyanya,pilipili na bidhaa nyingine pia wanalima maua yanayofukuza wadudu waharibifu na mimea mingine inayotumika kama tiba kwa binadamu,mimea na wanyama.

Alisema pia wamekuwa wakifuga nyuki, samaki, nguruwe,kuku ambao kwa pamoja hakuna wanaokuzwa kwa dawa za kemikali isipokuwa kutumia mimea ya shambani kwa kuwakinga na magonjwa mbalimbali huku nguruwe wakitumia ufugaji ambao hawatoi harufu wala kupiga kelele.

Mhando alibainisha kuwa katika shamba hilo wamekuwa wakiotesha mimea mbalimbali kwa teknolojia stahiki kiasi ambacho ipo ambayo ilikuwa haiwezi kuota katika maeneo hayo ya jagwani lakini kwa kutumia teknolojia ya kutandika plastiki nyeusi chini na kutandaza majazi yamestawi.

Alibainisha kuwa katika ukulima na ufugaji bila kutumia kemikali inatakiwa kufahamu matumizi ya miti ya asili kama dawa huku mbolea stahili inayotumika ni mboji ambayo katika kituo hicho wanatengeneza kwa kutumia majani.

MGOMBEA ubunge Jimbo la ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko, aliyekuwa Mwanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi