loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri- Tusitegemee mbegu kutoka nje

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga ameagiza wataalamu wa wizara na taasisi nchini kutumia utaalamu na uwepo wa fursa nzuri ya umwagiliaji kuzalisha mbegu bora kwa matumizi ya wakulima.

Alisema kauli hiyo juzi jijini Dodoma wakati alipofungua kikao kazi cha Menejimenti ya wizara, taasisi na bodi za mazao zilizo chini ya wizara ya Kilimo.

Hasunga alisema Tanzania haina haja ya kutegemea mbegu za mazao toka nje wakati ina eneo linalofaa kwa uzalishaji la kutosha na wataalamu wabobezi kwenye sekta ya uzalishaji mazao ya kilimo .

“Tunataka mbegu zizalishwe kipindi cha kiangazi kupitia kilimo cha umwagiliaji,ili wakati wa mvua wakulima wapande wala sio muda wa kuzalisha mbegu,” alisema.

Waziri Hasunga ametoa takwimu kuwa kwa sasa Tanzania inatumia tani 186,000 za mbegu ambapo uzalishaji ndani ya nchi ni chini ya tani 71,000 kwa mwaka hali inayosababisha kuendelea kutegemea mbegu zinazozalishwa nje.

Alitaja changamoto ya upungufu wa mbegu za miche ya chai,korosho ,michikichi, kahawa , mihogo na jamii ya mikunde hivyo kuchangia ukuaji mdogo wa tasnia za mazao hayo Waziri huyo wa kilimo aliwaeleza watendaji na watalaam wa wizara yake kuwa tayari Rais John Magufuli ameagiza kuwa nchi iwe na mkakati maalum wa kuongeza uzalishaji kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji.

Hasunga alisema katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli, wizara yake tayari imeagiza taasisi zake kutumia fursa ya umwagiliaji kuongeza uzalishaji mbegu nchini.

Alisema Tanzania ina eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hekta milioni 29.4 na zinazomwagiliwa hadi sasa ni hekta 475,000 tu hivyo wataalam wahakikishe mbegu zinazalishwa kwa wingi muda wote wa mwaka.

Wakati huo huo Waziri Hasunga ameonya dhidi ya kuongezeka kwa mbegu, mbolea na viuatilifu visivyo bora hali inayowaumiza na kusababisha hasara kwa wakulima nchini.

“Dawa na viuatilifu ambayo hayaruhusiwi kutumika yapo mengi sana. Hata mimi (Waziri) mwaka jana nilipigwa madawa yasiyo na ubora katika shamba langu Songwe na magugu hayakufa,” alitoa mfano Waziri Hasunga.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi