loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwakyembe aeleza umuhimu Bodi ya Ithibaki kwa waandishi

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ya Habari Mwaka 2016, huenda ikawaondoa hofu baadhi ya wanahabari waliopata elimu katika vyuo visivyotambuliwa na serikali.

Miongoni mwa majukumu ya bodi hiyo ni kuitazama tasnia ya habari nakuweka vigezo vinavyomtambulisha mwanahabari, kuwahakiki kulingana na sheria iliyopo na kuwapatia vitambulisho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema hayo wakati anazungumza na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro kuhusu uboreshwaji wa usikivu wa shirika la utangazaji la Taifa (TBC).

“Yapo mambo ya kiufundi yataangaliwa, mtu ana Shahada ya sheria, je naye akasome Diloma ya uandishi au nini kifanyike, hiyo ni kazi ya bodi, sasa itafanyaje kazi wakati mlifungua kesi kuipinga sheria husika,” alisema.

Akijibu moja maswali ya mwandishi wa habari hasa juu ya waliosoma katika vyuo ambavyo serikali haivitambui lakini vyenye mitaala ile ile inayofundishwa katika vyuo rasmi, waziri alijibu hiyo itakuwa jukumu la bodi.

Waziri alisema bodi itakayokuwa na wajumbe saba, akiwamo mkuu wa idara ya habari maelezo, wajumbe kutoka taasisi za elimu ya juu zinazofundisha uandishi wa habari, wawakilishi kutoka vyombo vya umma na binafsi na mwandishi mahiri, itatoa vigezo vya msingi ili kuhakiki elimu hiyo au vinginevyo. “Hili ni jukumu la bodi kulitazama kwa mapana yake, tayari serikalib imeweka sheria, jambo hili litatazamwa vyema na litawezekana, sheria siyo msahafu, leo mnataka muda wa ziada kupata Diploma utoke wapi, mlienda mahakamani,” alisema.

Dk Mwakyembe alisema sheria mpya itakayoanza Januari Mwaka 2022, imeipa hadhi taaluma ya habari ikilinganishwa na miaka iliyopita hivyo suala la wanahabari kwenda shule halikwepeki.

“Sheria mpya inataka mwanahabari akatiwe Bima ya matibabu na ile ya mazingira hatarishi ya kazi lakini pia kuwahakikishia kuwamo katika mifuko ya hifadhi ya jamii, haya hamuyaoni, mnabaki kusema sheria mbaya wakati nikiuliza wangapi wameisoma, nitapata majibu ya ajabu kabisa,”alisema.

Mmoja wa wanahabari alipendekeza waandishi kugawanywa katika madaraja na vigezo vya kufanya kazi ili kuruhusu hata wale wenye vyeti kufanya kazi isipokuwa wawe na mipaka ya maeneo ya kuandika habari.

“Katika taaluma nyingine zikiwamo za Uhandisi na Udaktari wapo watumishi kwa madaraja mbalimbali, wakiwamo Daktari, Mfamasia na Muuguzi na katika Uhandisi kuna Mhandisi na Mafundi wa kawaida wanaokunja nondo, na kila mmoja na wajibu wake….kwanini na uandishi usiwe hivyo?”alihoji.

TAKWIMU za udumavu ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Post your comments