loader
Picha

Katwila ahamishia makali Ligi Kuu

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema baada ya kungo’olewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), hasira zao wanahamishia kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa ambao ni mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2020, walitolewa kwa mikwaju ya Penalti 2-3 dhidi ya Sahare All Stars ya Ligi Daraja la Kwanza baada ya kumaliza kwa sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo kwenye Uwanja wa Gairo Shabib, Morogoro.

Alisema kutolewa na timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza sio ajabu, kwani mchezo wa mpira lolote linaweza kutokea na wamekubali matokeo, hivyo nguvu na akili yao wanajipanga kwa michezo ya Ligi kuhakikisha wanawania nafasi za juu.

“Ni kweli tumetolewa na Sahare sio wabaya wamepambana na kwa kuwa ni mechi ya mtoano chochote kinatokea tumekubali matokeo ingawa tumepoteza nafasi, lakini kasi na nguvu yetu tunaelekeza kujipanga na mechi za ligi kuhakikisha tunafanya vizuri huko,“ alisema Katwila.

Mtibwa kwa matokeo hayo, wanaungana na timu zingine za Ligi Kuu kama Mwadui FC, Mbeya City na Ruvu Shooting ambazo zimetupwa nje ya mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho la Azam, ambapo bingwa wake analiwakilisha taifa katika Kombe la Shirisho Afrika.

RAIS Dk John Magufuli ameiagiza Ofisi ya Rais Utumishi na ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi