loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

U 17 wako tayari kukutana Uganda

KOCHA wa timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17, Bakari Shime amesema baada ya kuitoa Burundi sasa anaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata.

Shime aliyasema hayo jana kwa njia ya simu akiwa Burundi na kusema anashukuru kwa ushindi wa bao 1-0 walilopata ugenini na kukiri mchezo ulikuwa mgumu.

“Tumefanikiwa kuitoa Burundi kwa mabao 6-1 ila mchezo wa jana (juzi) ulikuwa mgumu sana kwa sababu timu hizi zinajuana na tumekutana mara tatu katika kipindi cha miezi miwili,” alisema Shime.

Naye mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo, Protasia Mbunda anashukuru Mungu kwa kupata ushindi na kusema upungufu ni sehemu ya mchezo, hivyo wanaamini kocha wao atayafanyia kazi yote yaliyojitokeza katika mchezo huo.

“Matokeo yaliyopita tumeyafuta na tunaanza upya, mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wetu walijipanga vema kwa sababu walijua Tanzania ni timu ngumu,” alisema Protasia. Baada ya ushindi huo, Tanzania sasa itakutana na Uganda baada ya kuifunga Ethiopia 5-1 jana.

Juzi Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk Jilly Elibariki Maleko leo alipata chakula cha jioni na wachezaji hao kuwapongeza kwa ushindi.

Timu hiyo iliwasili jana saa 12 jioni ikitokea Burundi ambapo ilipata ushindi wa bao 1-0 na kusonga hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-1.

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments