loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha Sven alia na walinzi Simba

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na maendeleo ya safu yake ya ulinzi baada ya kufungwa bao kwenye michezo minne mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Akizungumza juzi kocha huyo alisema licha ya kufanikiwa kutinga kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la FA baada ya kuwang’oa Mwadui kwa mabao 2-1 kwenye mchezo ulichezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam bado anafikiria kuja na dawa itakayosaidia kuzuia hali hiyo.

“Tumepata ushindi kwenye mchezo wa leo (juzi) na tumefanikiwa kusonga hatua inayofuata ni jambo nzuri kwa timu, lakini kwangu binafasi bado sijafurahishwa na safu yangu ya ulinzi katika michezo minne iliyopita kila mechi tumeruhusu kufungwa bao na kinachoniumiza kichwa zaidi ni namna wanavyofungwa, “ alisema Sven.

Simba ukitoa mchezo dhidi ya Mwadui mechi zingine tatu ambazo Simba imefungwa licha ya ya kuibuka na ushindi ni pamoja na Alliance 4-1, mbele ya Mbao 2-1 na ule waliotaka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Yanga.

Alisema kinacho muumiza kichwa ni namna safu ya ulinzi inavyoruhusu kufungwa ni kutokana na kukosa mawasiliano na wakati mwingine wakishafungwa wanakuwa kwenye presha kubwa ya kutengeneza mazingira ya kutafuta bao la kusawazisha.

Sven alisema kwenye mchezo huo kuanzia sehemu ya kiungo walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kupata mabao lakini kukosekana kwa umakini sehemu ya mwisho ilisababisha kuchukua muda mrefu hadi kufanikiwa kupata bao la ushindi kupitia Francis Kahata.

Alisema ushindani walioupata kwenye mchezo ulipita ni maandalizi kuelekea kwenye mechi inayokuja ya ligi dhidi ya Coastal Union kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi kutengeneza mazingira ya kutetea ubingwa wa

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments