loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Wapuuzeni, msiwajibu'

RAIS John Magufuli amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi, wakaibebe nchi na kuisemea kwa mazuri huku akiwasisitiza kuwapuuza na kutowajibu wale wote wanaoichafua nchi.

Alisema pamoja na kwamba wapo wanaoichafua nchi kwa maslahi yao, lakini wanayoyataka yamekuwa yakishindikana kwani nchi imekuwa ikipokea misaada na kuendelea kujiendesha kama kawaida.

Rais Magufuli aliyasema hayo ikulu jijini Dar es Salaam jana wakati akiwaapisha mawaziri wawili akiwemo Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu, balozi wa Uswizi Maimuna Tarishi, balozi wa Japan Hussein Katanga na balozi wa Umoja wa Mataifa Marekani Kennedy Gaston.

Alikiri kuwepo kwa maneno mabaya dhidi ya nchi ikiwemo suala la ubaguzi katika elimu lakini yameshindwa kuletea nchi madhara.

“Nendeni mkiwa mmeibeba Tanzania, kitu chochote kinachohusu Tanzania mkakisemee, suala la elimu mtu wa Benki ya Dunia alikuja hapa alitoa pesa akijua sisi tunafanya nini. Acheni wale wanaopiga kelele waendelee, msiwe mnawajibu. Sisi tunajua tunachofanya,” alisema Rais Magufuli.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza kwenye hafla hiyo, aliwataka mabalozi hao walioteuliwa kuiwakilisha nchi kuwa mabalozi wazuri watakaoiwakilisha nchi vyema. Balozi Tarishi Geneva una mashirika zaidi ya 40 ya kusimamia na Vienna una mashirika saba. Tujaribu kuimarisha ofisi yetu kule Geneva,” alisema.

Alisema Februari 24, mwaka huu, kuna mkutano wa UMoja wa Mataifa wa haki za binadamu na kumtaka aweke mambo sawa juu ya masuala yanayozungumzwa vibaya juu ya Tanzania.

“Tutashirikiana kuhakikisha katika kikao hicho tuweke mambo sawa kwa jumuiya ya kimataifa. Kuna mambo yanapotoshwa, Sisi tunajali elimu ya wasichana wote. Serikali imekuja na njia mbadala hata kwa waliopata mimba kupata elimu. Hatubagui katika elimu. Kuna njia mbadala tunatumia na si ubaguzi kama ambavyo watu wanataka kuiaminisha dunia,” alisisitiza.

Alimtaka balozi anaenda Japan kuiwakilisha pia vyema nchi kwa kuwa nchi inauhusiano mzuri na Tanzania ikiwemo miradi inayoendelea baina ya nchi hizo mbili.

Wakati, Rais akitoa kauli hiyo, juzi Benki ya Dunia ilibainisha kuwa inafikiria kutoa mkopo kwa Tanzania wa dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya elimu nchini humo japokuwa kumekuwepo na maneno juu ya sera ya nchi kuzuiwa wanafunzi waliopata mimba kuendelea na shule za serikali.

Aidha, Kiongozi wa Chama cha upinzani cha AVT-Wazalendo Kabwe Zitto aliandika barua kwa benki hiyo akiitaka isitishe kutoa mkopo huo kwa kuwa utaleta ubaguzi kwa wanafunzi hasa wale waliopatiwa mimba.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi