loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maspika wastaafu kupewa majoho

 MKUTANO wa 18 wa Bunge la Kumi na Moja pamoja na kupokea na kujadili taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge pia utakabidhi majoho kwa maspika wastaafu watatu waliyokuwa wakiyatumia wakati wakiongoza Bunge.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema maspika watakaokabidhiwa majoho hayo ni pamoja na Pius Msekwa, Samuel Sitta kwa niaba yake mke wake Margareth Sitta na Anne Makinda.

"Katika Mkutano huu 18 wa Bunge kutakuwa na shughuli ya kukabidhi majoho kwa maspika wastaafu Pius Msekwa, Samuel Sitta (Marehemu) ambapo joho alilotumia litapokelewa na mke wake, Margaret Sitta kwa niaba ya familia, na Anne Semamba Makinda," alisema.

Spika Ndugai alisema shughuli hiyo itafanyika leo Januari 28, 2020 katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 18 wa Bunge mara baada ya kipindi cha maswali," alisema.

Alisema katika mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya Bunge kupokea na kujadili taarifa za mwaka za kamati, pia katika mkutano huo maswali 125 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na wabunge.

Pia wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo yataulizwa kwa Waziri Mkuu Alhamisi Januari 30 na Februari 6, mwakak huu.

Ndugai alisema katika mkutano huo pia Bunge litajalidi na kupitisha miswada miwili ya sheria ukiwemo wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba Nane wa 2019 na muswada wa sheria ya Usuluhishi wa mwaka 2020.

Katika muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho sheria 14 zikiwemo ya haki za watoto, mamlaka ya sheria za serikali za mitaa za wilaya na mikoa, ya uvuvi na ya viwanda vya nyama.

Pia katika mkutano huo taarifa za kazi za mwaka mzima za kamati 15 zitawasilishwa kwa mujibu wa masharti ya Kauni ya 117 (5) ambazo ni Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali, Hesabu za serikali za mitaa, Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Kamati ya Bajeti na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

"Kamati ya Miundombonu, Nishati na Madini, Ardhi Maliasili na Utaliii, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Huduma na Maendeleo ya Jamiii, Kamati ya Masuala ya Ukimwi, Sheria Ndogo na Katiba na sheria, kamati ya tawala na serikali za mitaa na mambo ya nje, ulinzi na usalama.

Mkutano huo wa 18 wa Bunge la kumi na moja unaanza leo Januari 28 hadi Februari 7, mwaka huu jijini Dodoma.

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi