loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyakazi TRA kupandishwa kizimbani

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) mkoani Dodoma, inatarajia kuwafikisha mahakamani watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa ya Sh milioni moja.

Rushwa hiyo inadaiwa walichukua kutoka kwa mfanyabiashara wa jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma, Sosthenes Kibwengo.

Alisema uchunguzi wa Takukuru umeonesha Januari 11, mwaka huu, majira ya mchana watuhu- miwa Emmanuel Ernest (31) na Vincet Hassan (29), wote wakiwa ni wafanyakazi wa TRA Dodoma wakiwa katika eneo la Majengo jijini Dodoma, walimkamata mwendesha mkokoteni akiwa na mzigo wa alminiamu kwa kosa la kuwa na risiti ya EFD ya tarehe ya nyuma na isiyo na thamani halisi ya mzigo walioukamata.

Kibwengo alisema baada ya kuushikilia mzigo huo, walirudi na mwendesha mkokoteni hadi kwenye duka la Maliki Tarimo lililopo maeneo ya CCM jijini hapa ambapo mzigo huo ulitoka na kuacha ujumbe kwa mwenye duka ambaye pia hakuwepo dukani kwake, uliomtaka kufika ofisi za TRA na pia wakaacha namba zao za simu.

Alisema mwenye duka aliwapigia simu watuhumiwa hao ambao walimtaka awape Sh milioni moja ili wasichukue hatua stahiki za kisheria dhidi yake.

Wakati huo huo, Mahakama ya wilaya ya Kongwa imemtia hatiani kwa makossa matatu Dickson Urio (52), ambaye ni Ofisa Mifugo mwandamizi wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa katika shauri la jinai namba 37/2018.

Urio amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 300,000 kila kosa katika makosa matatu ya matumizi ya nyaraka za kumdanganya mwajiri.

Ilidaiwa na Takukuru kuwa mtuhumiwa alitumia risiti za kughushi kumtaarifu mwajiri wake kwamba amenunua vifaa kwa ajili ya semina ya wafugaji, jambo ambalo halikuwa la kweli.

Vilevile Hakimu Kisasila Saguda alimwamuru mshtakiwa kuilipa halmashauri ya wilaya ya Kongwa Sh milioni 1.63 baada ya kutumikia adhabu yake.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi