loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samatta kuanza kazi EPL

NAHODHA wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta leo anatarajia kuichezea kwa mara ya kwanza Aston Villa tangu akuposajiliwa kutoka Genk ya Ubelgi.

Aston Villa inashuka dimbani kumenyana na Leicester City katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Carabao utakaofanyika kwenye Uwanja wa Villa Park, huku Samatta akitegewa katika safu ya ushambuliaji.

Samatta alisajili wa Aston Villa hivi karibuni huku akitegemewa sana na timu hiyo ambayo ilikuwa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu ya England.

Tayari kocha wa timu hiyo, Dean Smith amethibitisha kutaka kumpanga Samatta huku akiwa na matumaini makubwa na mshambuliaji huyo baada ya safu ya ushambuliaji ya Aston Villa kuwa na matatizo baada ya kukumbwa na majeruhi na wengine kuondoka katika timu hiyo.

Hata hivyo, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, anatarajia kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa beki kisiki Mturuki Caglar Soyuncu.

Aidha, mchezo huo ambao unatarajiwa kutazamwa na mamilioni ya Watanzani wengi baada ya Samatta kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika klabu ya Ligi Kuu ya England.

Licha ya Villa kupewa nafasi ya kuibuka na ushindi kwa faida ya uwanja wa nyumbani, bado mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote kutokana na matokeo ya mechi ya awali, ambayo walitoka sare ya 1-1, na ubora wa Leicester kwa sasa.

Kocha Smith aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Samatta amekuwa na mwenendo mzuri mazoezi tangu ajiunge na klabu hiyo, hivyo kuna nafasi kubwa ya kumchezesha katika mchezo huo wa leo.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments