loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JWTZ kujenga uwanja, jengo la bil 4.7/- Kinondoni

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa ujenzi wa uwanja wa mpira pamoja na jengo la utawala yenye thamani ya Sh bilioni 4.7.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta alisema hayo wakati wa kusaini mkataba huo na jeshi hilo.

Kabla ya kusaini mkataba huo, Sita alisema mwaka jana Baraza la Madiwani katika manispaa hiyo lilipitisha fedha za miradi mikubwa mitatu ambayo ni ya kiwanja cha mpira kilichopo eneo la Mwenge.

Pia stendi ya mabasi ya zamani iliyopo Mwenge pamoja na Jengo la Utawala ambalo linajengwa katika manispaa hiyo.

Alisema uwanja huo wa mpira utakaogharimu sh. bilioni 2.7, utasaidia masuala ya mpira pamoja na shughuli nyingine mbalimbali ambazo zitakuwa chanzo kizuri cha mapato kwa manispaa hiyo.

“Leo tumesaini mradi wa kiwanja cha mpira na jengo la biashara ambapo kiwanja cha mpira kinagharimu bilioni 2.7 na jengo la utawala linagharimu sh. bilioni 1.6, jumla yake ikiwa sh. bilioni 4.7,” alisema.

Akizungumzia hilo, Luteni Kanali David Luoga wa JWTZ kikosi namba 361 amesema, jeshi limeamua kuunga mkono juhudi za manispaa hiyo kwani wana ufanisi wa kutosha katika kufanya kazi hiyo.

“Manispaa kazi yenu kutuletea vifaa kwa wakati sisi tutajenga kwa wakati,” alisema.

Alisema ujenzi huo unaonyesha utafanyika kwa miezi nane lakini wao kama jeshi wataukamilisha ndani ya miezi sita kwani wapo tayari kufanya kazi usiku na mchana.

Alisema kwenye uwanja huo wa mpira kutakuwa na ghorofa moja na maduka 50, pia eneo la jukwaa la watu maarufu litakalochukua watu mpaka 20,000.

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi