loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba- Kauli ya Kabwili inachukiza

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imesema, kauli ya kipa wa Yanga SC Ramadhani Kabwili kuwa klabu hiyo ilitaka kumhonga gari apate kadi ya njano inachukiza na si ya heshima.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mbatha imeeleza kuwa, kauli ya Kabwili ina madhara makubwa kwa uadilifu wa klabu hiyo na viongozi wake.

“Klabu ya Simba inafurahishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania dhidi ya kauli kama hizi kwa vyombo husika. Klabu ya Simba inaamini kuwa jambo hili liko mbele ya mikono ya vyombo husika na litachukuliwa hatua stahiki kwa haraka” imeeleza taarifa za Mbatha.

Mbatha ameeleza kuwa, Simba imesikitishwa na kauli ya Kabwili aliyoitoa jana kwenye kituo cha redio cha East Afrika cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Simba inapinga na kukemea vikali kauli kama hizo kwa kuwa pia zinauweka mashakani uadilifu na heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Klabu ya Simba inaendelea kuweka juhudi zake kwenye miradi yake na ratiba za Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam”imeeleza taarifa hiyo.

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments