loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodi yamuonya mwamuzi aliyechezesha Simba v. Yanga

BAADHI ya waamuzi wa Ligi Kuu Bara akiwemo Jonesia Rukyaa aliyechezesha mechi ya Simba dhidi ya Yanga mapema mwaka huu wamepewa onyo na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka nchini kutokana na sababu mbalimbali.

Akitangaza uamuzi wa kamati ya Saa 72 mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam leo, kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwanyela ametangaza kuwa, Rukyaa na mwamuzi msaidizi ambao walichezesha pambano namba 31 la watani wa jadi mnamo Januari 4, mwaka huu, walishindwa kutoa maamuzi sahihi kwa baadhi ya matukio.

Hata hivyo, mpambano huo uliisha kwa sare ya 2-2 huku Yanga ikitoka nyuma kipindi cha pili na kusawazisha yote. Kwa upande mwingine, mwamuzi wa kati aliyechezesha mchezo kati ya Mbeya City na Yanga, Florentina Zablon kwa kushindwa kutoa uamuzi wa haki kutokana na hali ya uwanja iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mbali na hayo, Bodi hiyo imetoa ratiba ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara inayoonesha kuwa timu zitacheza katikati na mwisho wa wiki ili ligi hiyo imalizike kwa muda uliopangwa.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi