loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tumuige shuhuda huyu wa saratani

Katika gazeti letu la leo tumeandika habari inayohusiana na shuhuda aliyepona ugonjwa wa saratani ya titi, Anjela Kuzilwa, mwenye umri wa miaka 70.

Shuhuda huyo amewashauri wanawake nchini kuona umuhimu wa kuchunguza afya zao ili watakapobainika kuwa na ugonjwa huo waweze kuanza vipimo katika hatua za awali.

Yeye katika maeelezo yake, alisema amepatiwa mionzi 25 katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) jijini Dar es Salaam na kwa sasa ni mzima na anaendelea na maisha yake, ikiwa ni miaka 16 tangu kupata ugonjwa huo.

Kauli ya Anjela ambaye ni mwanzilishi wa asasi inayoshughulika na saratani ya Matiti (TBCF) ya jijini Dar es Salaam, ni habari njema kwa wote ambao wanasita kuelekea katika maamuzi hayo kwa sababu ya woga walio nao.

Aidha, maelezo hayo wakati tunaelekea maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani yatakayofikiwa kilele Februari 4, mwaka huu, tuna amini yatakuwa chachu kubwa kwa Watanzania hasa wanawake kuchukua maamuzi ya makusudi kuangalia mwenendo wa afya zao na kuwahi matibabu kabla hali haijaharibika.

Inafaa tukamwangalia shuhuda huyu na kutambua kwamba, maneno kwamba ukitibiwa saratani unakufa mapema ni matokeo ya kuchelewa kujulikana kwa hatua iliyofikia saratani hiyo.

Shuhuda huyu ametueleza kwamba, ametibiwa na kupona na anaamini kitendo cha wagonjwa wengi kubaki majumbani bila matibabu kinadhoofisha maisha ya watu hao.

Kutokana na maelezo aliyotupatia shuhuda huyo, ni vema kwa wananchi wengine kujinasua katika usingizi wa woga na kukubali hali ili kuweza kutibiwa mapema ikibainika tatizo.

Ni vema tukatambua kwamba, ukiambiwa una ugonjwa huo na ukaanza tiba mara moja unaweza kukaa zaidi na zaidi bila hofu ya kifo wala kifo chenyewe.

Tunampongeza shuhuda huyo kwa kujitolea kutoa elimu hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanawake wenye umri mkubwa na mdogo kutodharau kuchunguza afya zao ili kuwahi matibabu na uhakika wa mgonjwa kupona.

Hakika muda umefika kwa wanawake na watu wengine kubadilika na kuona kwamba uzima wao na kuendelea kuwa na furaha na familia zao kunategemea maamuzi yao ya kuikubali hali na kutibiwa.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi