loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF iyafanyie kazi madai ya rushwa Ligi Kuu Bara

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea na bingwa wake ndio huwa mwakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika huku bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam, yeye huwakilisha nchi katika mashindano ya Shirikisho Afrika.

Klabu za Tanzania kwa miaka mingi hazijafanya vizuri ukiiondoa Simba ambayo msimu uliopita iliondolewa katika hatua ya robo fainali, hatua ambayo ni kubwa. Ligi Kuu inashirikisha jumla ya timu 20, ushindani ukiwa mkubwa, ambapo Simba inayoongoza ikiwa na pointi 44 wakati timu inayofuata, Azam iko pointi tisa nyuma ya Simba. Simba imecheza mechi 17 wakati Azam wenyewe kwa mechi hizo wana pointi 35.

Hivi karibuni kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili alitoa tuhuma za kutaka kuhongwa na Simba, eti asicheze katika pambano la watani wa jadi lililofanyika mapema mwezi uliopita kwenye Uwanja wa TaifaDar es Salaam na timu hizo kutoka sare ya kufungana 2-2.

Kabwili alidai kuwa Simba waliahidi kumpa gari aina ya Toyota IST ili afanye kile wanachotaka ili wao wafaidike. Hizo ni tuhuma nzito na mbali na kuzitupa kwa Kamati ya Nidhamu tunadiriki kuwa hata Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ingehusika ili ukweli ujulikane na sheria zifuate mkondo wake.

Hilo si jambo dogo au la utani, kwani Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) pamoja na lile la Afrika (Caf) wamekuwa wakikemea na kupiga vita rushwa, hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liongeze umakini katika kulishughulikia hilo.

Na endapo itabainika kuwa Kabwili hana uhakika na kile akisemacho, basi mchezaji huyo naye achukuliwe hatua kali na klabu yake na hata TFF, ili iwe fundisho kwa wengine.

Lakini Kabwili alisema ama uhakika na kile alichozungumza, hivyo asipuuzwe asikilizwe ili ukweli ujulikane na hatua zichukuliwe.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: TAHARIRI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi