loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbwana Samatta: NYOTA YAKE YAZIDI KUNG’ARA | AJAZA KIJIJI MBAGALA

NYOTA ya kijana wa Mbagala, Mbwana Samatta imeendelea kung’ara baada ya Jumanne kuwa Mtanzania wa kwanza kuicheza Ligi Kuu ya England.

Ni jambo la ajabu kabisa kwa Mtanzania kucheza katika ligi kubwa na ya heshima kama ile ya England, kwani wachezaji wa Tanzania hawastahili kuichezea kutokana na kiwango cha chini cha soka cha nchi yetu.

Ligi Kuu ya England ina utaratibu wake, kwani mchezaji kutoka Tanzania au nchi yenye viwango vya chini kisoka, hawezi kusajiliwa moja kwa moja katika klabu inayoshiriki ligi hiyo.

KUSAJILIWA SAMATTA

Samatta alipata na- fasi hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa alionao, na uwezo wake wa kuisaidia Aston Villa kukwepa kushuka daraja na kingine kuwa mfungaji bora katika klabu yake ya Genk ya Ubelgiji.

Samatta pia ana kila sababu ya kuichezea Ligi Kuu ya England kwani wakati akiichezea Genk, aliifunga klabu kubwa kabisa duniani Liverpool, ambao sasa ni mabingwa wa Ulaya na Dunia. Lakini pamoja na ubora wa Liverpool, ambayo kwa sasa inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, Samatta aliifunga na kuweka historia kuwa Mtanzania wa kwanza si tu kucheza katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, pia kufunga katika michuano hiyo.

SHUJAA WA TAIFA

Samatta alianza kuichezea Aston Villa Jumanne wakati iliposhinda 2-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Carabao na sasa watacheza dhidi ya Man City katika fainali ya kombe hilo.

Mchezaji huyo ni shujaa wa taifa kwani Jumanne alipokuwa akiichezea kwa mara ya kwanza Aston Villa, uwanja wa Mbagala ulijaa mashabiki wa kila aina wakijitokeza kumshuhudia Samatta akiichezea timu hiyo.

Uwanja huo ulijaa kweli kweli na hata taarifa hizo zimewafikia mabosi wake Samatta kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, ambavyo viliripoti hali hiyo na kuelezea kuwa Samatta atia fora kwa watazamaji wengi Mbwana Samatta kujitokeza kufuatilia mchezo wa Villa na Leicester City.

Samatta alitupia katika mtandao wake wa kijamii watu kibao wakifuatilia pambano hilo la Jumanne lililofanyika kwenye Uwanja wa Villa Park. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, hivi karibuni alisajiliwa akitokea Genk na alianza katika mchezo huo walioshinda mabao 3-2, na alicheza kwa dakika 68 kabla ya kutolewa baada ya kuumia nyama za paja. “Hali nzuri kutoka nyumbani kwangu…, “anasema Samatta alipotupia katika mtandao wa Instagram.

Hata Aston Villa walipata muitikio wa kuungwa mkono na watu wa Tanzania na waliwashukuru kwa kujitokeza na kumuunga mkono Samatta na klabu hiyo. Huo ni uhamisho mkubwa kwa Tanzania tangu mchezaji huyo alipojiunga na Genk ya Ubelgiji, ambako alifunga mabao 76 na kusaidia mara 200 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

MCHEZO WA LIGI

Samatta anatarajia kuichezea kwa mara ya kwanza Aston Villa mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika leo dhidi ya AFC Bournemouth kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Vitality. Huo ni mchezo wa kwanza wa Samatta tangu ajiunge rasmi na Villa hivi karibuni katika dirisha dogo la usajili mwezi huu.

CARABAO CUP

Villa baada ya kuifunga Leicester City sasa itakutana katika fainali na Manchester City, ambao waliifunga Manchester United katika mchezo wa fainali. Man City iliifunga United kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa Jumatano usiku kwenye Uwanja wa Old Trafford baada ya kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.

Samatta sasa atakutana na Manchester City katika mchezo wa fainali huku akikabiliana na vigogo wengine katika mechi za Ligi Kuu ya England.

Samatta ameendelea kuwa kivutio na kipenzi cha wapenzi na wasio wapenzi wa soka nchini Tanzania, kitu ambacho kitawafaidisha mno Aston Villa ambao huko nyuma haikuwa na wapenzi wengi nchini, lakini sasa itasepa na kijiji kila itakapokuwa ikicheza.

Leo tena ni matarajio ya wengi kuwa wapenzi wengi wa soka watajitokeza katika uwanja wa soka wa Mbagala, ili kumshuhudia Samatta akikipiga tena na Villa, lakini sasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

MOJA ya shabaha ya kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ...

foto
Mwandishi: MWANDISHI WETU

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi