loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga Vs Mtibwa mechi ya kisasi

MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo wanashuka uwanjani kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga haitaisahau Mtibwa Sugar ilivyowafunga bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu msimu uliopita uliochezwa Aprili mwaka jana Morogoro.

Aidha, zimekutana tena msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi hatua ya nusu fainali na kutoka sare ya bao 1-1 lakini Mtibwa ikiifunga kwa mikwaju ya penalti 4-2 na kufuzu fainali.

Leo zinakutana katika mchezo wa ligi huku mashabiki wa Yanga wakitamba kulipa kisasi kwa sababu mara ya mwisho kukutana kwenye uwanja huo raundi ya kwanza msimu uliopita Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Timu hizo zinakutana Yanga ikitoka kupata ushindi ugenini katika mchezo uliopita kwa mabao 3-1 dhidi ya Singida United huku Mtibwa Sugar ikitoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja huo wa Taifa.

Yanga inashika nafasi ya sita kwa pointi 28 na Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya 10 kwa pointi 23 na yeyote ana anaweza kuibuka na ushindi kutegemea na alivyojiandaa kimbinu dhidi ya mpinzani wake.

Mechi hiyo inaweza kuwa ngumu kwa sababu mara nyingi zinapokutana kila mmoja hucheza kwa ushindani wa hali ya juu na wachezaji wa kuchungwa ni Bernard Morrison ambaye katika michezo miwili amefunga bao moja na kutoa pasi mbili,Yikpe Gnamien, David Molinga na kwa Mtibwa kuna Ismail Aidan, Japhari Kibaya ambao wamekuwa wakisumbua pia.

Mchezo mwingine Mbeya City itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Samora Iringa. Mbeya City iko kwenye mstari wa kushuka daraja ikiwa na pointi 13 huku Azam FC ikishika nafasi ya pili kwa pointi 36. Timu zote mbili zinahitaji matokeo mazuri Azam FC ikitaka kuendelea kubaki katika nafasi yake na Mbeya City kujiondoa hatarini.

LEO ndio fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi