loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TRA kuongeza ukusanyaji mapato Iringa

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefungua ofisi katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwa na lengo la kusogeza huduma kwa walipakodi ambao wallikuwa wakisafiri zaidi ya kilomita 40 kufuata huduma hiyo Iringa Mjini.

Aidha mamlaka hiyo imepanga kutumia ofisi hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi ili kuweza kufikia lengo la mkoa wa Iringa ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/20, mkoa huo uliwekewa lengo la kukusanya  Sh bilioni 71.3 kama kodi za ndani.

Akifungua rasmi ofisi hiyo juzi Ijumaa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asiah Abdallah alisema kufunguliwa kwa ofisi ya TRA katika wilaya yake ni hatua nzuri katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ya wilaya na mkoa kwa ujumla.

"Kusogezewa huduma za ulipaji kodi hapa wilayani kwetu kutachochea ari ya ulipaji kodi miongoni mwa wananchi na hatimaye kukuza uchumi wa nchi," alisema na kuongeza kuwa katika wilaya yake kuna raslimali nyingi ambazo zinasaidia kukuza uchumi kama vile kilimo cha mazao ya misiti, chai na matunda, ufugaji na utalii.

Hali kadhalika, aliwataka wananchi wake kusajili na kupata namba ya utambulisho wa Mlipakodi (TIN), kulipa Kodi stahiki kwa wakati, kutunza kumbukumbu za kibiashara, kutoa risiti kwa mauzo wanayofanya pamoja na kushirikiana na watumishi wa TRA kupata elimu ya kodi na kulipa Kodi kwa wakati.

“Natoa wito kwa wafanyabiashara wa wilaya yangu kutumia fursa hii adhimu ya uwepo wa ofisi ya TRA kupata elimu ya kodi na kulipa Kodi kwa wakati ili kukuza uchumi wa wilaya," alisema Asiah.

Naye Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Utawala wa TRA, Alice Lukindo ambaye alimwakilisha Kamishna Mkuu wa TRA alisema Mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia na kutekeleza sheria za kodi kwa kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato ya serikali na hivyo kufungua ofisi katika Wilaya ya Kilolo kunalenga kuongeza wigo wa walipakodi na huduma za ulipaji kodi kwa watanzania wengi zaidi.

Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Lamson Tulyanje alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/20 Wilaya ya Kilolo imepangiwa kukusanya jumla ya Sh bilioni 5.8 ikiwa ni asilimia 8.2 ya lengo la mkoa wa Iringa la kukusanya jumla ya Sh bilioni 71.3 kwa Kodi za ndani.

Meneja huyo alisem kuwa katika kipindia cha katika mwezi Julai 2019 hadi Januari 2020, mamlaka hiyo imeshakusanya Sh bilioni 2.1 (asilimia 65.86 ya lengo) kutoka wilaya ya Kilolo.

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Iringa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi