loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

5,000 wajifunza kutengeneza bidhaa

WATU zaidi ya 5,000 nchini wamenufaika na mafunzo Kampuni ya Smile We Care inayojihusisha kuwakwamua Watanzania kupitia ujuzi mbalimbali kwa kutengeneza bidhaa za biashara.

Msemaji wa kampuni hiyo jijini Dodoma, Jane Mwenda akizungumza wakati wa sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo yenye makao makuu jijini Dar es Salaam kuwa ujuzi wanaoutoa unasaidia ndoto za Rais John Magufuli kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025.

Mengi ya mafunzo ambayo wametoa ni utengenezaji wa sabuni, keki na bidhaa nyingine.

Akizungumzia sherehe hiyo ya mwaka mmoja, Jane alisema sherehe hizo zimeambatana na kukutanishwa kwa vijana zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania kupata mafunzo yatakayowezesha kujiajiri.

Alisema kampuni hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha wanamuunga mkono Rais Magufuli kuwainua Watanzania kutoka hali ya chini mpaka kufikia malengo huku wakianzisha viwanda vidogo vya ujasiriamali.

“Yapo makampuni ya kitapeli ambayo lengo lao ni kutapeli watanzania, ila sisi tumejikita kuinua uchumi wa Watanzania wakiwemo vijana na watu wazima ambapo wanachangia kiingilio cha elfu ishirini na tatu tu na kujifunza utengenezaji wa sabuni, batiki, keki, shampuu,mafuta ya kupaka, mishumaa, na vitu vingi,” alisema.

Aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwaunga mkono kutoa nafasi zaidi ya elimu ya ujasiriamali elimu kwa vijana ili wawafikie vijana wengi na hatimaye faida kwa Watanzania wote.

Erick Malek maarufu Dk Kodak kutoka jijini Dar es Salaam ambaye ni mshauri wa kampuni hiyo, alisema ipo haja kwa vijana kujitambua na kutokata tamaa kutimiza ndoto ya maisha yao.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Taji Julius alisema kampuni hiyo imekuwa fursa kwake kwani amepata faida kubwa katika kujikimu kwenye mahitaji madogo pale anapotengeneza bidhaa ndogondogo.

Alisema vijana hususani wana vyuo wanayo fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yenye manufaa badala ya kutumia kwa ajili ya mambo ambayo hayana tija.

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi