loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rwanda yatangaza bei ya mahindi

WIZARA ya Viwanda na Biashara imetangaza bei mpya ya mahindi katika msimu huu wa mavuno kuwa faranga 223 kwa kilo moja, ikiwa ni ongezeko la asilimia sita.

Bei hiyo mpya iliyopokewa kwa shangwe na wakulima, imetokana na kuwapo upungufu wa mahindi kuanzia Septemba, mwaka jana, mpaka Januari mwaka huu.

Upungufu huo unatokana na ukame ulioikumba nchi hiyo na kusababisha upungufu wa zao hilo msimu wa mwaka jana.

Mavuno ya mahindi katika msimu wa kwanza mwaka huu yalianza katikati ya Januari na utamalizika Machi, mwaka huu.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wakulima wa Mahindi Rwanda, Evariste Tugirinshuti, aliliambia gazeti la New Times kuwa, wameridhishwa na bei hiyo.

Alisema kwa wastani uwekezaji wa wakulima kwa hekta ni faranga 700,000 mpaka faranga 900,000, hivyo kutumia faranga 187 kuzalisha kilo moja ya mahindi.

Alisema uzalishaji wa mahindi katika msimu huu ni mkubwa kuliko msimu uliopita, licha ya kuwapo kwa mafuriko yaliyoathiri mashamba makubwa.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, ametoa ...

foto
Mwandishi: Kigali, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi